Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe akutana na menejimenti pamoja na watumishi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) katika ofisi za Bodi zilizopo Vertinary Kilimo 1 Ghorofa ya Kwanza ambapo alitembelea ofisi za watumishi wa Bodi na kusikiliza kazi na majukumu ya taasisi pamoja na changamoto walizonazo.
Katika taarifa yake Prof. Shemdoe ameeleza jinsi taasisi hii ilivyoleta mageuzi ya kiuchumi mara baada ya kuanzishwa kwa Mfumo wa Stakabadhi (Warehouse Receipts System) ambao umesaidia wakulima kuondokana na changamoto mbalimbali ikiwemo changamoto ya bei, ubora wa mazao, wizi n.k
Prof. Shemdoe ameeleza kuwa watumishi wa taasisi hii wanapaswa kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na kushirikiana na Taasisi nyingine zinazofanya kazi zinzoendana kwani Bodi ndio inayotegemewa na wakulima na wazalishaji wa bidhaa hasa kupitia utaratibu wa stakabadhi ghalani, mfumo ambao umeleta mapinduzi makubwa.
Ushirikiano ni muhimu kati ya Bodi, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Soko la Bidhaa na wadau wengine ambapo hii itasaidia kufanikiwa kwa mfumo na kutatua changamoto zinazojitokeza kwa sasa.
Mkurugenzi mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) ndugu. Odilo Majengo ameeleza kazi mbalimbali zinazofanywa na Bodi hii ambapo amesema kwa kiasi kikubwa mfumo wa stakabadhi ghalani umesaidia kuweka bei nzuri kwa wakulima, kuanzishwa kwa mifumo ya kitaasisi imara ikiwemo Soko la Bidhaa (commodity exchange) na uimarishaji wa Ushirika, mfumo pia umesaidia kuwezesha wakulima kuwa na akaunti kwenye taasisi za fedha na malipo yote kupitia benki, Mfumo umesaidia kuondoa changamoto ya mizani, vipimo sahihi na ubora kwa kiasi kikubwa.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, ndugu. Ludovick Nduhiye ameipongeza taasisi hii kwa kazi nzuri wanazofanya hasa ya kusimamia mfumo wa stakabadhi ghalani kwenye mazao kama korosho ambapo mfumo huu umekuwa tiba kwa changamoto nyingi ambazo zilikuwepo kabla ya mfumo.
 Katibu Mkuu Prof. Riziki Shemode akizungumza na watumishi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo ndugu Odilo Majengo na aliyekaa kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ndugu, Ludovick Nduhiye.
 Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) wakimsikiliza Katibu Mkuu Prof. Shemdoe (Hayupo pichani).
 Katibu Mkuu Prof. Riziki Shemdoe akiangalia baadhi ya ofisi za watumishi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) alipotembelea mapema leo. kulia ni Naibu Katibu Mkuu Ludovick Nduhiye, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji Ndugu Odilo Majengo.
 Naibu Katibu Mkuu Ludovick Nduhiye akizungumza wakati wa kikao na watumishi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) kushoto ni Katibu Mkuu Prof. Riziki Shemdoe.
 Baadhi ya watumishi wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) wakisilikiliza kwa makini maelezo ya Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Prof. Riziki Shemdoe (Hayupo pichani).
Mkurugenzi Mtendaji B odi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Ndugu Odilo Majengo  (Aliyesimama) akieleza kazi na majukumu ya Bodi hiyo kwa Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...