Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Godfred Mbanyi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kutanganza matokeo ya mitihani ya 19 ya bodi hiyo iliyofanyika kuanzia  tarehe 05 mpaka 08/11/ 2019.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB),  Godfred Mbanyi amesema Bodi hiyo haitavumilia endapo itamkuta Mtumishi yeyote anafanya kazi za Ununuzi na Ugavi na hajasajiliwa Kitaaluma na Bodi hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam wakati akitangaza matokeo ya Mitihani ya Bodi hiyo iliyofanyika Novemba 5 hadi 8,  2019,  Mbanyi amesema kuwa Watumishi katika fani ya ununuzi na ugavi lazima wasajiliwe Kitaaluma na Bodi husika.

"Ukikutwa Ofisini unafanya kazi bila kusajiliwa,  tunakupeleka Mahakamani, na usipofanya Mitihani ni kwa hasara yako mwenyewe",  amesema Mbanyi.

Katika hatua nyingine,  Mbanyi amesema kuwa Wanafunzi wengi wanafeli Mitihani hiyo kutokana na kushindwa kumaliza Mitaala,  hivyo kushindwa kujibu majibu sahihi. "Mfano wengi wanachukulia Hesabu ngumu,  suala ambalo si kweli",  amesema Mbanyi.

Wanafunzi waliofanya Mitihani ya Kitaaluma mwaka jana ni jumla ya Wanafunzi 1, 196 waliosajiliwa sambamba na Watahiniwa 1, 067 waliofanya mitihani husika ambapo ufaulu ulikuwa Watahiniwa 602 (56.4%) wamefaulu.

Wahatiniwa 441 (41.3%) waruhusiwa kukariri tena na Wahatahiniwa 24 (2.3%) wamefeli mitihani hiyo. Watahiniwa watatu wamefanya vizuri kwa ujumla katika ngazi za Professional Stage I,  III na utafiti.

Wanafunzi 10 wamefutiwa muda waliokuwa wamepewa kukariri na kuhakikisha masomo waliyokuwa wanadaiwa wamefaulu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...