Na MWAMVUA MWINYI,PWANI
RANCHI ya Ruvu ,Bagamoyo mkoani Pwani, imeongeza mapato yake kutoka milioni 50 kwa mwezi hadi kufikia makusanyo ya milioni 100 .
Aidha
imefanikiwa kuokoa kiasi cha sh .milioni 20 zilizotokana na upunguzaji
wa watumishi wasio wa lazima ,kujenga miundombinu imara isiyoongeza
gharama za kiutendaji na kupunguza matumizi yasiyo ya ulazima.
Kauli
hivyo imetolewa na meneja wa Ranchi ya Ruvu, Elisa Binamungu ,alipokuwa
anaelezea mafanikio ,maboresho na changamoto katika kipindi cha miaka
mitano .
"Fedha hii ya mapato imeongezeka kutokana na mauzo ya nyama ,ngozi ,tozo za vitalu na wanyama wadogo " anasema Binamungu .
Aidha
anaeleza, Ranchi ya Ruvu ilikuwa ikikabiliwa na changamoto kubwa ya
migogoro ya ardhi baina yake na wananchi ,uvamizi wizi wa mifugo ya
Ranchi na ufugaji holela hali ndani ya kipindi cha miaka mitano ambapo
changamoto hizo zinaelekea kuwa historia.
";Hii
hali ilisababishwa na tatizo la kutokuwa na mipaka na alama
zinazoonyesha eneo la Ranchi ambapo baada ya kuwekwa alama hizo tatizo
la migogoro hiyo limepungua ."
Binamungu
anasema, kuweka alama za kudumu kutenganisha maeneo ya Ranchi na jamii
kumesaidia kupunguza migogoro ya ardhi sanjali na kutenga eneo la hekta
20,000 ambalo limepimwa vipande vya hekta 500 na kupatikana vitalu 40
vinavyotumika kwa wafugaji wadogo ili kupunguza pia mifugo holela mkoani
hapo .
Anaeleza
,wanahamasisha kuanzia ngazi ya kijiji ,kata lengo mifugo inayoingia
ndani ya Ranchi iingie kwa utaratibu maalum ikiwa ni pamoja na kila heka
moja mfugaji anailipia tozo 3,500 kwa mwaka"
Hata
hivyo ,anaelezea kwamba ,nyama wanauza ya kiwango ,kilo moja 7,000
,wana duka la nyama katika Ranchi na jingine Dar es salaam ,wanauza kwa
wateja mmoja mmoja ,jumla na kwa wasambazaji kwa wenye mahitaji .
Binamungu alitaja malengo yao kuwa ni kuboresha miundombinu zaidi ili kujiimarisha ,kujenga machinjio ya kisasa .
Lengo
jingine ni kuongeza uzalishaji wa mifugo ya maziwa kwani wamegundua
kuna fursa kubwa ya uuzaji maziwa baada ya soko kupanda la maziwa huku
kukiwa na upungufu wa maziwa .
Tunahitaji
kuanzisha mashamba darasa ,hii ni Ranchi kubwa mashamba darasa
yatasaidia kuwaongezea ulewa wafugaji kufuga na kuondokana na uchungaji
,wa kufuga kiholela ,kienyeji ,ni wajibu wao kufuga kisasa .
Binamungu
anatoa wito kwa wafugaji kujiunga vikundi vidogo ili kuomba maeneo
katika Ranchi hiyo ili pia kupunguza migogoro na wakulima kwenye maeneo
yao .
Ranchi ya Ruvu ,ilianza mwaka 1957, kwasasa ina jumla ya wafanyakazi 43, mifugo ya ng'ombe 1,500 ,mbuzi 400 na kondoo 780.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...