Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Juni 24, 2020 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilitangaza kununua Madini ya Tanzanite yenye uzito wa 9.2kg na 5.8kg yenye thamani ya Shilingi Bilioni 7.8/- kutoka kwa Mchimbaji mdogo, Saniniu Laizer huko mkoani Manyara.

Baada ya Serikali kununua Madini hayo kutoka kwa Mchimbaji huyo mkoani Manyara, Katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Michuzi TV imekutana na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya amesema Serikali imefanya hivyo kutokana na sababu kuu tatu ambazo ni alama ya utajiri, alama ya ufahari kuwa mzalishaji wa Madini hayo na alama ya kuwa Jiwe kubwa la Tanzanite duniani.

Prof. Manya amesema awali Jiwe hilo la Tanzanite lilinuliwa nchini Thailand lilikuwa na uzito wa Kg 3.5 na nchi hiyo kujivunia ufahari wa Kivutio cha Utalii nchini humo.

"Sisi ndio wazalishaji wakubwa wa Madini haya, kwa hiyo tukiruhusu yanunuliwe na Mtu mwengine anaweza akatumia huo mwanya kupata umaarufu ambao tunastahiri sisi wenyewe", Prof. Manya.

Prof. Manya amesema jambo la kwanza Serikali iliamua kuhakikisha Madini hayo yanabaki hapa nchini ili iwe mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na yanunuliwe kwa bei ya Soko kwa maana kununuliwa kwa bei hiyo kwa yeyote aliyetaka kununua.
Katibu Mtendaji huyo amesema lengo la kununua Madini hayo,  ni fahari kwa Watanzania juu ya uwepo wa Madini ya Tanzanite katika nchi yao. Amesema uwepo wa Madini hayo ni alama ya utajiri na alama ya uzalishaji pekee nchini.
Mchimabji Mdogo wa Madini, Bilionea Saniniu Laizer akiwa ameshika Madini ya Tanzanite,ambapo moja lina kilo 9.2.Madini hayo yalinunuliwa na Serikali ya Tanzania kwa Shilingi Bilioni 7.8/-
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya akizungumza na Michuzi katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba akizungumza kuhusu Madini ya Tanzanite kununuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 Mchimabji Mdogo wa Madini, Bilionea Saniniu Laizer akionesha Hundi baada ya kuuza Madini hayo kwa Serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...