Na mwandishi wetu, Mbeya
SHIRIKA la umeme Tanzania TANESCO kupitia idara ya masoko, limeendelea na kampeni kabambe ya kuhakikisha inatoa Elimu kwa wachimbaji wadogo, kati na wakubwa wa madini pamoja na mashine za kusaga nafaka mkoani mbeya ili wafahamu Elimu ya matumizi Bora ya umeme.
Lengo la kampeni hiyo Ni kuhamasisha matumizi bora ya umeme, usalama wa umeme kwa  viwanda hivyo, kuunga mkono jitihada za Mh Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha uchumi wa viwanda unafikiwa kwa Kasi nchini na kuongeza Tija kwa Taifa.
Miongoni mwa migodi ambayo imekwishatembelewa mkoani Mbeya ni pamoja na mgodi wa makaa ya Mawe Kiwira, mgodi wa dhahabu Chunya wa Mdimi investment, Mehrab minerals resources, mgodi wa mama Today iliyoko wilayani Chunya.
  MaafisaTANESCO wakipata maelezo kutoka kwa Afisa madini wa kiwanda Cha Mdimi investment kilichoko wilayani Chunya mkoani Mbeya Joseph Mamuya wakati maafisa hao walipotembelea kiwandani hapo jana.
 MaafisaTANESCO wakipata maelezo kutoka kwa Afisa madini wa kiwanda Cha Mdimi investment kilichoko wilayani Chunya mkoani Mbeya Joseph Mamuya wakati maafisa hao walipotembelea kiwandani hapo jana.
 Mitambo ya kuchakata makaa ya mawe
 Maafisa wa TANESCO wakiwa kwenye moja ya viwanda walivyotembelea
Afisa mwandamizi wa ufundi kutoka TANESCO Stewartness Makiko akikagua moja ya mota zinazotumiwa na kiwanda Cha kukamua alizeti Cha Moravian kilichoko Wilaya ya chunya
 Mchimbaji mdogo wa dhahabu akisafisha mchanga kusaka madini hayo
 MaafisaTANESCO wakipata maelezo kutoka kwa Afisa madini wa kiwanda Cha Mdimi investment kilichoko wilayani Chunya mkoani Mbeya Joseph Mamuya wakati maafisa hao walipotembelea kiwandani hapo jana.
Vijana kutoka kiwanda Cha kuchakata mbao kutoka Tukuyu Cha Kapinga wakisikiliza kwa making Elimu inayohusu masuala ya umeme wakati walipowatembelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...