NA BALTAZAR MASHAKA, Mwanza

NI VIGUMU kuamini lakini inawezekana baada ya familia ya mzee Omari Bilal, mkazi wa Nyamhongolo katika Manispaa ya Ilemela, kupata msaada wa makazi ya kudumu.

Familia hiyo hivi karibuni ilipata changamoto ya ukuta wa nyumba yao iliyojengwa kwa matofali ya tope kuanguka kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha mfululizo kwa miezi kadhaa na bahati nzuri hakuna madhara ya kibinadamu yaliyotokea kwenye familia hiyo.

Kutokana na changamoto hiyo Taasisi ya The Desk & Chair Foundation (TDCF) Tawi la Tanzania liliamua kujenga nyumba bora ya kuishi ya gharama nafuu na kuikabidhi kwa familia hiyo.

Akikabidhi nyumba hiyo kwa mzee Bilal, Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Alhaji Sibtain Meghjee, alisema kuwa iliamua kubeba jukumu hilo baada ya kuguswa na changamoto ya familia hiyo kuwa katika hatari kuangukiwa na nyumba kwa sababu kuta zake hazikuwa imara baada ya upande mmoja kuanguka.

“Taasisi yeti ilichukua maamuzia ya kumjengea nyumba bora ya gharam nafuu ya vyumba vitatu, sebule, jiko, bafu, choo na kufunga mfumo wa umeme jua.Nyumba hii imegharimu sh. milioni 15 tu ambapo ujenzi umekamilika na leo tunaikabidhi kwa familia hii iweze kujistiri na kuendesha maisha yao,”alisema.

Mwenyekiti huyo aliwashukuru wafadhili waliotoa msaada wa fedha zilizotumika kwenye ujenzi wa nyumba hiyo na kuiwezesha familia ya mzee Bilal kupata makazi bora ya kudumu na kuondokana na tishio la kuangukiwa na kuta za nyumba yao ya awali ambayo pia imekarabatiwa.

Kwa upande wake mzee Bilal aliushukuru uongozi wa The Desk & Chair kwa kujali na kutambua changamoto iliyokuwa ikiikabili familia yake na kwamba hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu kwa moyo wao wa huruma. Aidha baadhi ya majirani wa familia hiyo Beata John na Paul Bubinza waliipongeza taasisi ya The Desk & Chair kwa jinsi inavyoshughulikia na kutatua matatizo ya jamii bila kubagua na kwamba familia hiyo ilikuwa kwenye mtihani mzito wa kuangukiwa nyumba lakini sasa maisha yamebadilika baada ya kukabidhiwa nyumba mpya ya kisasa.
 Nyumba ya awali ya familia ya mzee Omari Bilal baada ya ukuta wa upande mmoja kuanguka kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha kote nchini.
 Mwenyekiti wa The Desk & Chair Foundation, Alhaji Sibtain Meghjee (kulia) baada ya kumkabidhi nyumba Omari Bilal (kushoto).Nyumba hiyo yenye vyumba vitatu, sebule, choo, bafu na mfumo wa umeme jua imejengwa na taasisi hiyo kwa gharimu sh. milioni 15.

Picha na Baltazar Mashaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...