Katibu Tawala wa Wilaya ya Iramba Sango Songoma akiongea na jumuiya ya
Shule ya Sekondari ya Lulumba (hawaonekani pichani) baada ya kukabidhiwa
miundombinu na vitakasa mikono kwa ajili ya matumizi ya shule. Lulumba
ni moja ya shule iliyofanya vizuri katika masomo ya Sayansi kitaifa hapa
nchini.
Picha ya pamoja kati ya Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya
Lulumba, Uongozi wa Wilaya ya Iramba na Wataalam wa Wizara ya Maji baada
ya hafla fupi ya kuikabidhi shule hiyo vifaa na miundombinu ya kunawa
mikono shuleni hapo wilayani Iramba,
Kwa niaba ya Katibu Mkuu – Mkurugenzi Msaidizi, Wizara ya Maji Mhandisi
Lyidia Joseph (kushoto), akikabidhi kitasamkono, kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mwalimu Lino Mwageni, ikiwa
ni sehemu ya msaada wa miundombinu ya kunawa mikono na vitakasamikono
kutoka Wizara ya Maji katika jitihada za kutunza afya za wanafunzi wa
Shule ya Sekondari ya Lulumba.
Picha
ya pamoja baina ya Wataalam wa Wizara ya Maji, na Walimu wa Shule ya
Seondari ya Lulumba baada ya kukabidhiwa vifaa vya kujikinga na
maambukizi ya COVID 19, pia kuimarisha usafi wa wanafunzi wakati wote
baada ya shule kufunguliwa.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...