*Dirisha la Uchukuaji fomu kwa Wabunge na Madiwani laanza Julai 4.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
CHAMA cha United Democratic Party, (UDP) kimesema kitanuunga mkono Rais John Magufuli endapo Chama chake kikimpitisha kuwa mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Kimesema Chama hicho kimefungua dirisha la wagombea Ubunge na Udiwani kuanza kuchukua fomu katika Ofisi zao.
Mwenyekiti wa Chama hicho,John Cheyo (Mapesa) amesema kipaumbele cha Rais Magufuli kuwainua wanyonge na kuleta maendeleo nchini ndio sababu iliyowafanya kuwaunga mkono.
"Namsifu Magufuli kuweka Mazingira mazuri hospitali karibu na wananchi,kutuimarishia miundombinu ya Barabara na Reli," amesema na kuongeza kuwa
"Tumeamua kumuunga mkono Rais Magufuli endapo atapitishwa na Chama chake ila kama wasipompitisha tutatathimini kwanza ni nani tumpitishe alafu tutakuja na majibu kwa wananchi," amesema
Pia amesema wamefungua dirisha la uchukuaji wa fomu leo na siku ya mwisho wa uchukuaji wa fomu hizo watatangaza kuendana na ratiba ya Tume ya Uchaguzi (NEC).
"Natoa Rai kwa wanachama wa UDP, kuja kuchukua fomu ili kuweza kupata nafasi ya kuingia katika baraza la maamuzi," amesema

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama United Democratic Party John Cheyo akizungumza kuhusiana na uchaguzi mkuu na hatima ya chama hicho kuunga mkono mgombea urais wa CCM.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...