Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet
Maselle wa pili kushoto akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri
ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia wakati wakikagua
maendeleo ya ujenzi wa vivuko vya Bugorola Ukara na Chato Nkome katika
tukio lilofanyika katika yadi ya Songoro. Ujenzi wa vivuko hivyo
unategemewa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu, ujenzi huo
umechelewa kukamilika kama ilivopangwa kutokana na kutokea kwa ugonjwa
wa mafua makali maarufu Covid 19. Kulia ni meneja wa TEMESA Mwanza
Mhandisi Hassan Karonda na kushoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro
inayojenga vivuko hivyo Major Songoro.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet
Maselle akisoma taarifa ya ujenzi na ukarabati wa karakana ya TEMESA
mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya
Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia katika tukio lililofanyika
katika karakana hiyo. Kushoto ni meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi
Hassan Karonda na kulia ni mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mtakwimu
Bi. Suzan Ndunguru.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet
Maselle aliyenyoosha mkono akimuonyesha maendeleo ya ukarabati na ujenzi
wa majengo mapya ya karakana ya mkoa wa Mwanza Mwenyekiti wa Bodi ya
Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia wakati
alipotembelea karakana hiyo kujionea ujenzi unavyoendelea. Kulia ni
meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Hassan Karonda.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet
Maselle kulia akimueleza jambo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala
huo Prof. Idrissa Mshoro wa pili kulia wakati alipotembelea karakana
hiyo kujionea maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa karakana hiyo
unavyoendelea. Wa tatu kulia ni meneja wa TEMESA Mwanza Mhandisi Hassan
Karonda.
Muonekano wa kivuko ambacho kitatoa huduma kati ya Bugorola na Ukara
ambacho kinaendelea kujengwa katika yadi ya Songoro iliyopo Ilemela,
kivuko hicho pamoja na vivuko vya Mafia na Nyamisati na Chato Nkome
vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle
kushoto, Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala huo Prof. Idrissa
Mshoro katikati na Mkurugenzi wa kampuni ya Songoro Major Songoro
wakipita pembeni ya kivuko kinachotarajiwa kutoa huduma kati ya Bugorola
na Ukara wakati walipokua wakikagua maendeleo ya ujenzi wa vivuko
ambavyo vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti mwaka huu. Tukio
hilo lilifanyika katikayadi ya Songoro iliyopo Ilemela.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA MWANZA)



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...