Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

Unywaji wa Maji kwa wingi na vimiminika kama Maziwa, Uji na Sharubati (Juice) angalau Lita tatu kwa siku kumetajwa kuondoa Chumvi (Madini) inayozalishwa mwilini ambayo inatengeneza Mawe katika mwili wa binadamu, matumizi ya Vyakula kama Spinachi na Karanga za aina mbalimbali huzalisha Madini ya Calcium Oxalate (Mawe ndani ya Figo).

Hayo yameelezwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji Mfumo wa Mkojo na Uzazi kwa Wanaume katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. David Sylivester Mgaya wakati wa Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mgaya ameeleza kuwa kutokana na maradhi hayo, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili inafanya zoezi la uvunjaji wa Mawe kutoka kwenye Figo kwa kutumia Mashine bila kuweka jeraha lolote au maumivu katika mwili wa Mgonjwa, amesema unywaji Maji mengi unaruhusu uchafu wote (Madini, Chumvi) ambavyo havihitajiki mwilini vinatoka kwa Mfumo wa Mkojo.

Dkt. Mgaya amebainisha kuwa ugonjwa huo unaathiri zaidi jinsia ya Kiume (Wanaume) kuliko jinsia ya Kike (Wanawake), idadi imetajwa kufika Wanaume watatu kwa Mwanamke mmoja kutokana na Wanaume kuzalisha zaidi Madini ya Calcium Oxalate kwa wingi tofauti na Wanawake.

"Kama kuna mzibo kwenye Mfumo wa Mkojo, Mawe yanaweza kutengenezwa pia, kwa sababu Mfumo wa Mkojo unahusisha Figo, Mirija ya Mkojo ambayo inatoa Mkojo kwenye Figo kule kwenye Kibofu na Bomba pia".

"Tunashauri unywaji wa Maji mengi kwa sababu Mfumo wa Mkojo unaweza beba Jiwe dogo kulitoa nje ambalo chini ya Mil 10. Jiwe likifika Mil 10 hizo ni vigumu kusafiri kwenye Mfumo wa Mkojo", ameeleza Dkt. Mgaya.

Daktari huyo ameeleza kuwa kipindi cha nyuma upasuaji ulifanyika kutoa Figo kwa Wagonjwa kati ya wanne kwa mwezi,  lakini kwa sasa hizi huduma kwa Wagonjwa wengi ianfanyika bila upasuaji, na inafanyika kwa Mashine mpya kutokana na uwepo wa Vifaa Tiba.

DALILI ZA UGONJWA HUO
Maumivu ya tumbo haswa sehemu za pembeni ambazo zinakaribia na mbavu, Maambukizi mara kwa mara kwenye Mfumo wa Mkojo, Mgonjwa anaweza kupata Kichefuchefu na hata kutapika kama Jiwe limeziba kabisa Mfumo wa Mkojo, Pia Mgonjwa kukojoa Damu.

JINSI MASHINE INAVYOVUNJA MAWE KWENYE FIGO
Mashine inatumika kuvunja Jiwe ambalo ni kubwa (Vunjavunja) kuwa katika hali ndogo ambapo linaweza kubebwa na Mfumo wa Mkojo na kutolewa nje.

Mashine hiyo inatoa Mawimbi Mstuo ambayo yanafika mwilini yanatikisha mwili sehemu za Viungo vya Mwili na Jiwe hivyo Upokeaji wa mawimbi wa Kiungo cha mwili na Jiwe ni tofauti.

Jiwe hilo litapokea mawimbi kwa wingi zaidi kiasili Jiwe ni gumu, litacheza kwa nguvu zaidi kuliko viungo vya mwili vinavyoweza kucheza (Jiwe litavunjika kutengeneza chembechembe na ukinywa maji unatoa hizo chembechembe nje.

Mashine hiyo inatumia Mawimbi Mstuo ambayo ina vifaa au ina sehemu kubwa nne mpaka tano:-
1. Kitanda cha Mgonjwa.
2. Jenereta kuzalisha Mawimbi (inatumia Magnetic inazalisha Mawimbi.
3. Sehemu yakungalia Jiwe ndani ya mwili (Fluoroscopy) kuonyesha Jiwe au UltraSound.
Daktari Bingwa wa Upasuaji Mfumo wa Mkojo na Uzazi kwa Wanaume katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,  Dkt. David Sylvester Mgaya akiwaeleza Wananchi waliofika kwenye Banda la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhusu Mashine inayotumika kufanya upasuaji wa Mawe bila kuweka jeraha lolote na maumivu.
 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...