Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Linda Riwa (mwenye fulana nyeusi) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa mabingwa wa ligi ya Tanzania VPL Simba Sc mara baada kutawazwa kuwa mabingwa wa msimu wa 2019/2020 kwenye uwanja wa Majaliwa Ruangwa Lindi jumatano iliyopita. Vodacom Tanzania ndio mdhamini mkuu wa Ligi hiyo. 

………………………………………

Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania, PLC, ambaye ni mdhamini mkuu wa ligi kuu ya Vodacom Premier League (VPL) wameipongeza timu ya Simba Sports Club kwa kutwaa ushindi wa VPL 2019/2020. Pia kampuni hiyo imezipongeza timu zote zilizoshiriki VPL msimu huu. 

“Tunajivunia sana kuwa sehemu ya ligi kuu ya Tanzania bara kwani inaendelea kukua na kuboreshwa mwaka hadi mwaka. Pongezi zetu pia ziwaendee viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) , bodi ya ligi , vilabu vyote shiriki, waandishi wa habari, wadhamini wenza pamoja na Watanzania wote kwa ujumla kwa kushiriki kikamilifu katika ligi kuu mwaka huu,” Linda Riwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom alisema. 

Mpira wa miguu ni mchezo pendwa na muhimu sana hapa nchini na duniani kote.

Hii ni katika kuwapa burudani wateja wa Vodacom na watanzania kwa ujumla, kutoa nafasi za ajira kwa wachezaji na watendaji pamoja na kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa jamii na nchi tofauti. Mtandao wa Vodacom umekuwa mstari wa mbele katika kuwaunganisha na kuwaleta pamoja Watanzania kupitia mtandao namba moja na wenye kasi zaidi hapa nchini. Vodacom inasifika kwa kutoa huduma bora zaidi za data , kupiga simu, sms na mpesa. 

“Kama mnavyojua mpira wa miguu ni fursa kubwa ya ajira kwa vijana na tunafurahi na kujivunia kuwa sehemu ya mafanikio tunayoyaona kutokana na udhamini wetu ambao umewezesha baadhi ya wachezaji kama Mbwana Samatta na Simon Msuva kupata fursa za kucheza nchi za nje na kufika ulaya,” aliongeza Linda ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania. 

Vodacom kama wadhamini wakuu wa ligi kuu wametoa hamasa kwa klabu zote kuendelea kuwa mabalozi wazuri na kuwlezea nia ya kuendelea kutoa hamasa na ushirikiano kwetu kuendeleza michezo na hasa mpira wa miguu nchini. 

Vodacom pia inatoa shukrani za dhati kwa Watanzania kwa kuendelea kujitokeza kushabikia timu zao maana mchezaji wa kumi na mbili katika timu yoyote ya mpira ni mashabiki. “Shukrani zetu kwa waandishi wa habari kwa mchango mkubwa wa kuwahabarisha wapenzi wa mpira wa miguu walio ndani na nje ya nchi na kutangaza ligi yetu ya Vodacom Premier League,” aliongeza Riwa.
   

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...