WACHEZAJI wa Timu ya Taiifa, Taifa Stars, wameelezea kufurahishwa na udhamini wa Bia ya Serengeti Premium Lager na kwamba udhamini huo umekuwa chachu kubwa kwa mafanikio ya timu.

Mshambuliaji wa Taifa Stars John Bocco,  amesema udhamini wa Bia ya Serengeti umeiwezesha timu kupiga hatua kubwa ikiwa ni pamoja na kufuzu kucheza Mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka jana, baada ya miaka 39 tangu ifuzu mara ya mwisho.

“Mpira unahitaji uwekezaji ili kupata mafanikio. Kampuni ya bia ya SBL kupitia bia yake ya Serengeti imeweza kutoa udhamini ambao umekuwa chachu kubwa katika kuiimarisha timu yetu ya taifa. Pengine kama siyo udhamini huu tusingeweza kufika hapa tulipofika leo,” anasema.

Kampuni ya SBL kupitia Bia ya Serengeti ilikuwa mdhamini mkuu wa timu ya taifa kuanzia mwaka 2017 baada kusaini mkataba wa miaka 3 na Shirikisho la Mpira wa Miguu hapa nchini (TFF).

Kwa upande wake Frank Domayo, kiungo wa timu ya taifa anasema mdhamini pia amefanikiwa kujenga umoja na uzalendo kwa mashabiki jambo ambali limekuwa likiwapa hamasa kubwa wachezaji.

“Mdhami amefanya kazi kubwa kuwaleta Watanzania pamoja na kuhamasisha uzalendo kwa timu yao ya taifa kupitia vyombo vya habari na kampeni zinazowahusisha wachwzaji moja kwa moja,” alisema.

Pia Domayo anasema mdhamini amekuwa akifanikisha maandalizi mazuri kwa kuhakikisha kuwa mahitaji ya wachezaji na timu kwa ujumla yanapatikana kwa uhakika na kwa wakati pia.
‘Tumeona tofauti kubwa wakati bia ya Serengeti ikiwa mdhamini wa timu yetu ya taifa.

"Tumekuwa tukikaa kwenye hoteli nzuri tunaposafiri na tunapokuwa kambini n ahata maslahi yetu sisi wachezaji yameboreshwa kwa kiasi kikubwa jambo ambalo limetufanya tujitume zaidi,” anasema.

Wakati huo huo beki wa kulia wa timu hiyo Erasto Nyoni anasema mdhamini kwa kiasi kikubwa amekuwa karibu na wachezaji jambo ambalo limekuwa likiwatia moyo. "Mdhamini amekuwa na timu siyo tu ndani ya uwanja bali hata nje ya uwanja kwa kutupa hamasa na hili limekuwa likiwajenga vyema wachezaji kisaikolojia,”.

Naye mlinda mlango wa timu hiyo Mechata Mnata alisema mdhamini amekuwa akijitahidi kuipa timu kila aina ya ushirikiano na hivyo kufanya maandalizi yawe mazuri na kuweza kufanya vizuri katika mechi zake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...