WACHUNGAJI wa kanisa la Mlima wa Moto tawi la Buza, jijini Dar es Salaam, Patience Sunga (53) na mke wake Michou Sunga (50)  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka moja la kuishi nchini bila kibali.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Shija Sitta mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Richard Kabate imedai washtakiwa walitenda kosa hilo   Mei 3, 2019 huko Ilala jijini Dar es Salaam.

Imedaiwa siku ya tukio washtakiwa ambao ni raia wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo walikamatwa wakiishi nchini bila ya kuwa na kibali huku wakijua kufanya hivyo ni kosa na kinyume cha sheria.

Washtakiwa wote wamekiri kutenda makosa yao na kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 8 mwaka huu wa 2020 kwa ajili ya kuja kusomewa maelezo ya awali
Aidha katika kesi nyingine, wanamuziki watatu raia wa Congo Credo King, Yanick Makanga na Ombeni Pierre Kongo na Mchungaji wa kanisa la Ebeneza Gospel Church la Mbagala Jeremia ILunda wamefikishwa mahakamani hapo kujibu shtaka la kuishi nchini bila kibali.

Imedaiwa na Mwendesha mashtaka wakili wa serikali Godfrey Ngwijo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu kuwa Juni 9, 2020  huko Mbagala Kuu  katika Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam washtakiwa hap Pierre, Makanga na Yanick wakiwa raia wa Kongo Kongo walikutwa wakiishi nchini bila kibali.

Katika shtaka la pili imedaiwa siku na mahali hapo mshtakiwa Jeremia alikutwa akiwahifadhi washtakiwa hao wakati wa Kongo huku akijua kuwa wapo nchini kinyume cha sheria.

Washtakiwa wote wamekiri makosa yao na  wamehukumiwa kulipa faini ya Sh. 500,000 au wakishindwa watatumikia kifungo cha miaka mitano gerezani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...