Na Said Mwishehe,Michuzi TV

*Mwenyewe asema kura alizozipata ana deni la kulipa kwa Watanzania

Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Rais Dk.John Magufuli amewashukuru wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kwa kupitisha jina lake kwa asilimia 100 kupeperusha bendera ya Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu na kwamba kura ambazo amezipata zinampa nguvu ya kuendelea kuwatumikia kwa Watanzania kwa nguvu zake zote.

Dk.Magufuli amesema hayo Mjini Dodoma mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu  alipokuwa akitoa shukrani baada ya jina lake kupitishwa kwa kura 1,822 sawa na asilimia na kwamba hakutegemea kupata asilimia 100."Lazima niseme na mimi nimejipigia,ni ukweli sifahamu nitumie neno gani, wajumbe wa mkutano mkuuu mmenipa heshima kubwa, nina deni kwa watanzania.

"Kura ambazo nimezipata zisinipe kiburi, kura nilizopata leo zikanipe nguvu ya kuwatumikia watanzania hasa wanyonge,kura ambazo nimezipata leo zinipe nguvu ya kuwatumikia watanzania wote bila kujali dini,rangi wala kabila.Kura ambazo nimezipata leo nina deni kubwa kwenu, kura hizi ni heshima kwa CCM ,ni heshima kwa Watanznaia wote,"amesema Dk.Magufuli.

Ameongeza anafahamu kazi ya urais inahitaji msaada wa Mungu,hivyo ameomba Watanzania kuendelea kumuombea ili afanye kazi yake vizuri huku akitumia nafasi hiyo kusisitiza kwamba Tanzania ni nchi tajiri, ina kila kitu na kila aina ya rasilimali."Tunayo madini, tuna maji ya kutosha, tukisimamia vizuri tutatoa mchango mkubwa sana katika maendeleo.

"Kwa hiyo ndugu zangu wajumbe ambao mmehudhuria mkutano huu, CCM ndio Chama kinachoweza kuleta maendeleo katika nchi yetu, ndio maana nasema kura hizi ambazo mmenipa zikawe fundisho kwangu,zikawe fundisho kwa wasaidizi wangu na wale ambao watachaguliwa wajue kuna deni la kuwatumikia watanzania,"amesema Dk.Magufuli.

Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kuwaambia wajumbe hao kuwa wanapoondoka kwenye mkutano huo wasione wamemaliza kutokana na kupata kura hizo kwa asilimia 100 bali utakapofika wakati wa kampeni zifanyike kampeni za nguvu ili kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo."Nazungumza haya kwa kuamini sisi wote kwa umoja wetu tuhakikishe tunashinda.

"Pia wale ambao wameonesha nia ya kugombea naomba muendelee kuwa wamoja, kuna tabia ya mgawanyiko baada ya kura za maoni na matokeo yake tunasababisha Chama kushindwa.Nawapongeza waliokuwa walioshiriki mchakato wa kugombea urais Zanzibar kwani wameendelea kuwa wamoja na wote wako hapa na watamuunga mkono na kushiriki kikamilifu mgombea urais Zanzibar Dk.Hussein Mwinyi,"amesema Dk.Magufuli mbele ya wajumbe hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...