NA MWAMVUA MWINYI ,PWANI
BAADHI
ya wakulima kijiji cha Kitonga na Kidogozero ,kata ya Vigwaza ,Chalinze
mkoani Pwani ,wamelalamikia tabia ya wafugaji kuingiza mifugo yao
kiholela katika mashamba yao na kusababisha kula mazao na kuwasababishia
hasara .
Wamesema
vitendo hivyo vimekithiri hivyo wameomba uongozi wa kata ,wilaya na mkoa
kuendelea kusimamia kero hiyo ili waishi kwa amani .
Katibu
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)tawi la Kidogozero,Vera Sultan Mindu
alisema ,tatizo hilo walishawahi kulitolea taarifa wilaya na mkoa na
kijiji kilijiwekea sheria ndogondogo lakini wafugaji wamekuwa wakiingiza
mifugo kiholela na kunyanyasa wakulima hata wakiwa wanajaribu kuwaeleza
makosa yao .
Akizungumza
wakati akitoa kero hiyo wakati diwani anaemaliza muda wake ,Mohsin
Bharwani alipokwenda kuwaaga rasmi na kutoa taarifa ya utekelezaji ya
kijiji na kata ,Vera alisema wafugaji hawaogopi hata kushtakiwa polisi
hali ambayo inawakatisha tamaa wakulima .
";Wapo
wafugaji ambao wamenunua maeneo kijijini hapo lakini ni ya kujenga na
kuishi na sio kufuga ,unakuta wao wanafuga na kero zaidi ipo kwa
wafugaji wanaoitana kutoka maeneo ya nje na kijiji hicho "; Vera
alifafanua .
Bharwani
alifanya mkutano wa aina hiyo pia kijiji cha Kitonga ambako ,mwenyekiti
wa kijiji hicho ,Enock Mhingo ,alisema wamechoshwa na wafugaji
,wanaingiza mifugo katika mashamba .
" Kuna changamoto nyingine ya barabara ya Ruvu -Kitonga kutopitika vizuri hasa nyakati za mvua ya masika,tuna mahitaji pia ya umaliziaji wa vyumba vya madarasa matatu shule ya msingi Kitonga na zahanati "alisema Mhingo.
Nae
mfugaji anaeishi kijiji cha Kitonga almaarufu Lake ,alieleza ni kweli
tatizo lipo ,na kama serikali kupitia kamati za maridhiano wakisimama
kidete tatizo litaisha.
Alisema ,kuanzia sasa watakuwa wakiwakemea hasa wafugaji wanaotoka nje ya kijiji ili waishi kwa amani na wakulima .
Diwani
anaemaliza muda Vigwaza ,Mohsin alitoa wiki moja kwa TAKUKURU Chalinze
iende ikachunguze tatizo kijiji cha Kitonga ambacho sheria ndogo zipo
lakini wafugaji wanaonekana kuwa na nguvu .
Mohsin
,aliomba viongozi wa kijiji kuacha kupindisha sheria ndogondogo
walizojiwekea ,na kulinda kundi lenye pesa ,kwa kufanya hivyo
wanasababisha kundi linalonyimwa haki kuishi bila raha na kwa hasara .
"
Kuweni makini viongozi wenzangu wa vijiji ,simamieni wananchi hawa kwa
haki ili kulinda amani na waishi kwa upendo pasipo chuki na migongano
,:!alisisitiza Mohsin .
Mohsin
alichangia mifuko ya saruji 100 na matofali 2,000 katika ujenzi wa
shule ya msingi Kitonga na mifuko ya saruji 50 itakayoelekezwa ujenzi wa
zahanati.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...