Mwanafunzi wa Uhandisi wa Vifaa Tiba, mwaka wa kwanza katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Innocent Douglas akionesha kifaa cha Ventilator kinavyofanya kazi kwa mtu aliyeshindwa kupumua.

Wanafunzi wa Uhandisi wa Vifaa Tiba, mwaka wa kwanza katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Innocent Douglas na Aiche Rogers wakiwa katika Picha ya pamoja na Kifaa cha Ventilator katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Uhandisi wa Vifaa Tiba, mwaka wa kwanza katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), Innocent Douglas na Aiche Rogers wakionesha Ventilator hiyo kwa baadhi ya Wananchi waliofika kushuhudia Kifaa hicho katika maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
WANAFUNZI wa Uhandisi wa Vifaa Tiba, mwaka wa kwanza katika Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wameunda kifaa maalum kinachomsaidia Binadamu kupumua kinachojulikana kwa jina la Ventilator.
Akizungumza na Michuzi TV katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam, Mwanafunzi wa Taasisi hiyo, Innocent Douglas amesema Kifaa hicho (Ventilator) ina mfumo unaoruhusu hewa kuingia na kutoka na inafanya kazi kama Mapafu ya Nje.
Innocent amesema Kifaa hicho kinatoa msaada zaidi sehemu za Vijijini sehemu ambazo upatikanaji wa hewa ya Oxygen ni mdogo, amesema Kifaa hicho kina uwezo wa kuzalisha Oxygen zaidi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Viwanda katika Taasisi hiyo ya DIT, Dkt. John Msumba amesema wanafaya kazi kubwa kuhakikisha Wanafunzi wanaohitimu Chuoni hapo wanafanya kile kinachotakiwa kufayika Viwandani kupitia dhana ya kutoa Wahitimu watakao tatua matatizo ya Jamii (Teaching Factory Concept).
Dkt. Msumba amesema Wanafunzi hao wameunda Kifaa hicho baada ya kuona kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa Mashine ya kusaidia kupumua, amesema Wahadhiri wanatoa muongozo lakini kazi kubwa inafanywa na Wanafunzi wenyewe.
"Kiukweli Tanzania tuna Wanafunzi wana uwezo mkubwa sana, na wanafanya vitu vikubwa sana, hawa wanaweza kubomoa hii Ventilotor na kuunda upya bila shaka yoyote", amesema Dkt. Msumba.
Amesema Kifaa hicho kama kitaagizwa nje ya nchi ni gharama kubwa zaidi sambamba na Vifaa kutoka nje ya nchi, kuwa na matatizo makubwa, amesema wanatatua matatizo ambayo Jamii ina uhitaji mkubwa.
Dkt. Msumba amesema DIT inataka kuwa Chuo kikubwa cha Dunia (MIT of Africa) amesema wana malengo hayo na kuwa Chuo kinachoongoza kutatua matatizo kwa Jamii.
Kifaa hicho kinatumika katika Vituo vya Afya kwa matibabu zaidi, kutoa msaada wa kupumua kwa Binadamu. Wazo la Wanafunzi hao kuunda Ventilator hiyo ni kutokana na kuenea Virusi vya Corona (COVID-19) vinavyosababisha kushindwa kupumua vizuri.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...