Mvumbuzi wa mashine ya kutakasa mwili, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Alex Malisa akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya 44 ya biashara  yanayofanyika katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
CHUO kikuu cha Dar es Salaam, waungana na watanzania wote katika kupambana na Virusi vya Corona (Covid-19) hapa nchini kwa kutengeneza Mashine ya kutakasa mwili bila kugusa kifaa chochote (Disfection tanel).

Akizungumza na Michuzi blog jijini Dar es Salaam katika Maonesho ya 44 ya Biashara, Mvumbuzi wa mashine ya kutakasa mwili, Chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Alex Malisa amesema kuwa mashine hiyo  imebuniwa katika kitengo cha uhandisi Viwanda katika chuo kikuu cha Dar es Salaam kwaajili ya kupambana na virusi vya Corona vinavyotesa mataifa mengi hapa dunia.

"Wazo la kuvumbua mashine hii lilikuja kwenye msimu ambao tulikumbwa na janga la Corona, moja ya njia kubuni na kuendeleza mashine ya kutakasa mwili mzima."

"Hii hutumika hata katika hospitali mbalimbali baada ya madaktari kufanya Oparesheni (au Upasuaji) huwa wanajitakasa kama walikuwa wanamfanyia upasuaji mtu ambaye alikuwa anamaradhi yanayoweza kuambukizwa kwa njia ya hewa kwahiyo wanapita katika mashine hii ili kujitakasa mwili mzima." Amesema Malisa.

Hata hivi baada ya kuendeleza wazo la kutengeneza mashine hii tukapata ufadhili wa kuitengeneza kutoka kitengo cha uzalishaji uhandisi wa viwanda katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam.

"Hii sio mashine ya kwanza kutengeneza ya kwanza tulitengeneza kwaajili ya majaribio pale pale chuo baada ya kuona imefanya kazi vizuri ndio wakatufadhili tena kwaajili ya kutengeneza mashine nyingine." Alisema Malisa.

Amesema kuwa mashine hiyo inagundua yenyewe kama kunamtu na inatoa Sanitaiza ambayo pia imetengenezwa na chuo kikuu cha Dar es Salaam
Baada ya hapo inaanza kutoa Sanitaiza.

Kila pawapo nakitu changamoto hazikosekani Malisa amesema kuwa changamoto kubwa wanayokumbana nayo kutokuwa na mtaji mkubwa wa kununua bidhaa na vifaa mbalimbali zinazoweza kutengeneza mashine hizo kwa wingi zaidi na ili ziweze kuwafikia watu wengi zaidi duniani kote kwaajili ya kupambana na janga hili la Corona na magonjwa mengine yanayoambukuza kwa njia ya hewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...