Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam ya Chuo kikuu Mzumbe Profesa Honest Ngowi akitoa mafunzo kwa wataalamu na wakufunzi wa vyuo mbalimbali hapa nchini kuhusu kwenda kidijitali katika masuala ya manunuzi na Ugavi.

Na Avila Kakingo, Globu ya jamii
WATAALAM wa masuala ya Ugavi nchini waaswa kuendana na ukuaji wa teknolojia nchini na kuendana na dunia ya kidigitalj ilivyo, mifumo yao iende kidijitali na wafanye biashara kidijitali.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Teknolojia ya kidijitali katika Mnyororo wa Manunuzi na Ugavi, Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Honest Ngowi, amesema kuwa wasioendana na teknolojia watapitwa. 

"Washiriki wa mafunzo haya lazima nao waendane na mabadiliko na wawe na uelewa wa dunia ya kidijitali ilivyo lazima mifumo yao iendane na teknolojia wafanye biashara kidijitali, lasivyo watapitwa na maendeleo yanayokuja duniani." Amesema Profesa Ngowi.

Amesema kuwa zamani ilikuwa lazima uwe na bohari kubwaa, lakini baada ya kwenda kidijitali sio lazima kuwa na bohari kubwa ili uweze kufanya biashara.

Hata hivyo Profesa Ngowi amesema kuwa wataalamu wa masuala ya ugavi wajaribu  kwa kila namna ili kuendana na mapinduzi makubwa ya teknolojia yanayofanyika duniani kote.

 Licha ya kwenda kidijitali katika masuala ya ugavi Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam hawapendi mtu yeyote aachwe katika dunia ya kidijitali wa ugavi na wapo tayari kutoa mafunzo ya teknolojia ya kidijitali ili kuendana na malengo ya milenia ya hakuna mtu ataachwa nyuma katika nnyororo wa Ugavi.

Kwa Upande wake  Mwakilishi Mkazi wa taasisi la Kuehne Foundation, Betrice  Milu,  amesema kuwa taasisi ya Kuehne wanafanya kazi ya kusaidia Wakufunzi pamoja na wataalamu wa masuala ya mnyororo wa manunuzi na ugavi hapa nchini.

Amesema kuwa wameshafanya semina mbalimbali kwaajili ya kuwajengea uwezo wadau wa ugavi kwani kumekuwa na mafanikio makubwa kwani washiriki wanajitokeza kwa wingi.

Beatrice amesema kuwa wataalamu wa masuala ya ununuzi na ugavi wameweza kutoa changamoto wanazozipitia ili kuweza kuandaa mafunzo mengine na kuangalia ni nini kinahitajika kuendana na dunia ya ununuzi ugavi inavyoelekea.

"Katika kushirikiana na Chuo Kikuu Mzumbe tumeona ushiriki umekuwa mzuri kwani tumepata washiriki wengi na mafunzo yanaonesha mlengo chanya katika masuala mazima ya myororo Manunuzi na Ugavi." Amesema Beatrice.

Kwa upande wa Mratibu  wa Mradi wa Kuehne, Chuo Kikuu Mzumbe, Daktari, Omary Swalehe amesema kuwa mafunzo haya yanatolewa kwa taasisi za umma na taasisi binafsi ili kuweza kuboresha shughuli za Mnyororo wa manunuzi na ugavi hapa nchini. 

"Tumeleta mafunzo ya teknolojia ya kidijitali katika mnyororo wa Manunuzi na ugavi kwa sababu dunia ndiko inakoelekea.

Manunuzi na ugavi sio Kisiwa  nayo inaendana na mabadiliko ya sayansi na Teknolojia." Amesema Dkt. Omary.

Amesema wamelenga kuwawezesha wataalamu kupata elimu ya kidijitali katika masuala ya manunuzi na ugavi ili kuweza kuboresha  ufanisi katika kazi zao.

Dkt. Omary ametoa wito kwa Wataalamu  wa manunuzi na ugavi kushiriki fursa za mafunzo  yanayotolewa bure chuoni hapo ili wasiachwe nyuma katika kazi zao.
Mtoa maada, Albogast Musabila akizungumza wakati wa kutoa mafunzo ya ukuwaji wa teknolojia katika masuala ya Manunuzi na ugavi jijini Dar es Salaam leo.



Mshiriki akitolea ufafanuzi jambo.
 Baadhi ya washiriki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...