Na Amiri Kilagalila,Njombe

Katibu mkuu ofisi ya Rais Dokta Moses Kusiluka ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya uongozi wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) amewaonya watakaosababisha kuwepo kwa kaya hewa zinazonufaika na mpango huo awamu ya tatu baada ya kukamilika kwa uhakiki unaofanyika nchi nzima.

Dokta Kusiluka ametoa onyo hilo alipozulu mkoani Njombe katika mtaa wa Uwemba na kuzungumza na walengwa wa TASAF wakati wa zoezi la uhakiki likiendelea na kwamba mkono wa sheria hautamuacha yeyote atakayehusika kuingia katika mpango huo ilihali hana sifa.

“Kwa hiyo ikitokea kiongozi amefanya hivyo,hatua za kisheria zitachukuliwa kwasababu ni ubadhilifu na hatua zitachukuliwa kwa kiongozi na muhusika anayekuja kuchukuwa fedha,hayo ni maelekezo ya Mh,Rais”alisema Dokta Moses Kusiluka

Baadhi ya walengwa wa TASAF katika mtaa wa Uwemba mkoani Njombe akiwemo Ostakia Ndawala na Selina Nyakalua wanakiri kuwa TASAF imewasaidia sana kwenye mambo ambayo walikuwa hawawezi kushughulikia kama kuwapeleka watoto shule na hata kuendeleza shughuli za ufugaji.

“Tulikuwa maskini sana lakini tulipopewa zile hela tayari uwemba tunakula parachichi,tuna kuku na sasa hivi tunaendelea vizuri,mkampe salam sana Rais kwa kutukumbuka kwenye mradi huu, na sisi tuko nyuma yake na safari hii tunataka apite tena” Alisema Selina Nyakalua

Selestin Mwanyika ni mwenyekiti wa mtaa wa Uwemba anasema awamu moja ya uhaulishaji fedha walizopata walengwa katika mtaa wake zimeonesha mafanikio makubwa huku akiwataka endapo watapata fedha nyingine baada ya uhakiki wazielekeze katika malengo mahususi.

“Tangia naingia madarakani wamepata mara moja na sikuona matatizo yoyote,lakini tuliona mafanikio wengi wamefuga kuku,na wengine wamefuga nguluwe japo kwenye Nguruwe huku kuna myumbo” alisema Selestin Mwanyika

Jumla ya wanufaika 132 wa TASAF katika mtaa wa Uwemba wameendelea kuhakikiwa ili kujiridhisha kama wana sifa zinazohitajika katika mpango huo lengo la serikali likiwa ni kutaka kuondoa kaya hewa ili zisalie kaya sahihi katika mradi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...