Na Mwandishi Maalumu
 Leo Julai 1, 2020 Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi kwa mara ingine amesimamia zoezi  la usafirishaji wa dharura (repatriation) ya  Watanzania pamoja na raia kadhaa wa nchi hiyo waliokwama nchini humo kutokana na "Lockdown" na kusitishwa safari za ndege inayoendelea huko.

Balozi Milanzi amesimamia  zoezi hilo lililohusu usafirishwaji wa jumla ya abiria 60, ikiwa ni Watanzania 44 na raia wa Afrika Kusini 16,  ambao wanarudi kufanya kazi kwenye makampuni na taasisi za nchi hiyo baada ya kukwama huko kwa miezi kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ubalozi wa Tanzania nchini humo, abiria hao wamesafirishwa kwa ndege ya kukodi ya kampuni ya Precision Air, hilo likiwa na zoezi la nne kufanyika nchini humo t
okea ugonjwa wa COVID 19 uikumbe dunia na kupelekea nchi nyingi duniani, ikiwemo Afrika Kusini, kusimamisha kila kitu ikiwemo safari za kuondoka nchini mwao.


 Tayari Tanzania imeshafungua  anga lake na kuruhusu utalii pamoja na safari za ndege za kimataifa viendelee kama kawaida, ambapo tayari mamia ya watalii wameendelea kumimimika nchini, huku wengine wakitarajiwa kuwasili kwa wingi baada ya mashirika ya ndege ya kimataifa kuanzisha safari zao.

 Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Meja Jenerali (Mst) Gaudence Milanzi akiagana na Watanzania pamoja na rais wa Afrika Kusini wakati aliposimamia zoezi la kuwasafirisha kwa dharuran katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa O.R. Tambo jijini Johannesburg leo. Chini ni taswira mbalimbali za abiria hao wakielekea kupanda ndege kurejea Tanzania leo. 








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...