TUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imevitaka vyama vya siasa na wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu kama sehemu ya kufurahia haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa kuzingatia misingi ya amani na utulivu kama njia ya ustaarabu katika kujenga demokrasia ya kweli.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Mathew Mwaimu wakati wa ufunguzi wa kikao cha mashauriano kuhusu mkakati wa kuwa na uchaguzi jumuishi na wa amani wenye ushirikishwaji mkubwa wa wanawake, vijana na watu wenye Ulemavu uliofanyika leo jijini Dodoma.
Mwaimu amesema kuelekea uchaguzi huo ni muhimu kama Taifa kukumbuka kuwa amani ya Nchi ni tunu ambayo imekuepo kwa muda mrefu toka uhuru na inapaswa kulindwa kwa wivu mkubwa.
Amezitaka Taasisi za Kiraia, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Msajili wa Chama, Ofisi ya Waziri Mkuu na Tume ya Uchaguzi ambao ni wadau wa kikao hiko kuhakikisha wanaelimisha umma na kuyasaidia makundi hayo kupata ufumbuzi wa matatizo yao.
" Mtakumbuka Rais Dk John Magufuli wakati akivunja Bunge Juni mwaka huu alisisitiza kuhusu uchaguzi kuwa huru na haki lakini aliwaonya watu wenye nia mbaya ya kuvuga uchaguzi hivyo na mimi niwaombe watanzania kukataa kuwa sehemu ya watu watakaovuruga amani yetu, " Amesema Mwaimu.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi amesema uchaguzi wa mwaka huu unawapa matumaini makubwa kwamba Wanawake, Vijana na Walemavu kujitokeza kwa wingi kuomba nafasi za uongozi na kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya utekelezaji wa mikataba ya kikanda na Kimataifa juu ya usawa wa kijinsia na maendeleo.
Amesema pamoja na changamoto zilizopo, uchaguzi wa mwaka huu unakuja wakati Tanzania ikiweka rekodi kwa mara ya kwanza ya kuwa na Makamu wa Rais mwanamke (Mama Samia Suluhu Hassan) katika uchaguzi wa mwaka 2015 na uwepo wa mgombea Urais ambaye alikua Mama Anna Mghwira.
" Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazofanya vizuri katika ushiriki wa wanawake katika uongozi, takwimu zinaonesha hadi Januari 2019 tulikua tunashika nafasi ya pili Afrika Mashariki na nafasi ya 25 duniani kwa kuwa na wanawake wabunge 36% hata hivyo bado hatujafikia lengo la kuwa na asilimia 50/50.
Hata hivyo TGNP tuna matumaini makubwa kuhakikisha wabunge wanawake wa majimbo wanaongezeka ndani ya Bunge letu kwa mwaka huu na tumeanza kuona uelekeo na mwitikio wa wanawake katika kuomba nafasi hizo," Amesema Lilian.
Nae Mkurugenzi wa Kituo cha Amani, Haki na Msaada wa Kisheria (PLAJC), Jaruo Karebe amesema kikao hiko ni cha mashauriano na mikakati ya kuhakikisha mazingira wezeshi na kuimarisha ushiriki wa wanawake, vijana na walemavu katika mchakato mzima wa uchaguzi.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mathew Mwaimu akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha mashauriano kuhusu mkakati wa kuwa na uchaguzi jumuishi wenye ushirikishwaji wa Wanawake, Vijana na Walemavu.
Wadau mbalimbali walioshiriki ufunguzi wa kikao cha mashauriano kuhusu mkakati wa kuwa na uchaguzi jumuishi wa Wanawake, Vijana na Walemavu wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Kituo cha Amani, Haki na Msaada wa Kisheria (PLAJC), Jaruo Karebe akizungumza katika mkutano huo wa kujadili ushirikishwaji wa Wanawake, Vijana na Walemavu katika uchaguzi mkuu ujao.
Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Liliana Liundi akizungumza katika mkutano huo wa kujadili ushirikishwaji wa Wanawake, Vijana na Walemavu katika uchaguzi mkuu ujao.
Wadau mbalimbali walioshiriki kikao cha pamoja cha kujadili mashauriano kuhusu mkakati wa kuwa na uchaguzi jumuishi wenye ushirikishwaji wa Wanawake, Vijana na Walemavu leo jijini Dodoma.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...