Na Woinde Shizza , ARUMERU
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Idd Hassan Kimanta amewasimamisha kazi Mtendaji Kijiji na kata ya Mwandeti na Afisa Tarafa ya Mukrati kuwa chini ya ungalizi ili kupisha uchuguzi zaidi na hatua kali zitachukuliwa baada ya uchunguzi kukamilika.

Maamuzi hayo yamefanyika katika kikao kazi kati ya Mkuu wa Mkoa na maafisa tarafa Watatu wa halmashauri ya Meru, watendaji wa kata 26 na vijiji 90 pamoja na wakuu wa idara na vitengo katika halmashauri hiyo.

Aidha Kimanta alisema kuna uzembe mkubwa umefanyika katika utendaji wa majukumu yao, hasa kushindwa kudhibiti kilimo cha bangi katika maeneo yao.

“Haingii akilini bangi inalimwa kwa miezi 3 na mwezi wa 4 inavunwa wewe mtendaji wa kata na kijiji upo hapo na hauchukui hatua yoyote”.

Alisema haieleweki kwanini nyie kama viongozi mmeshindwa kudhibiti kilimo cha bangi kwa muda wote huo na mpo hapohapo.

Aliwataka watumishi kuacha kufanyakazi kwa mazoea kwani dhama hizi ninza kuwajibika kila mtu kwenye nafasi yake.

Kimanta alisisitiza zaidi kwa viongozi wa kata na vijiji kuwafichua wote wanaolima bangi katika maeneo yao badala ya kuwaficha, amesema kwa kufanya hivyo wanachangia kuiharibu jamii.

Aliwataka viongozi hao wa kata na vijiji kutatua kero za wananchi katika maeneo yao hivyo watakuwa wamewatumika vyema wananchi wao.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Arumeru Mkuu wa Wilaya hiyo Jerry Muro, alisema tatizo kubwa kwa watumishi wa wilaya hiyo ni kufanya kazi kwa mazoea ndio maana wanashindwa kuchukua hatua mbalimbali za kiutendaji katika maeneo yao.

Aidha, Muro aliwataka watumishi wote kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali wawe wabunifu zaidi katika kutekeleza majukumu yao badala ya kuwasubiria viongozi wa ngazi ya juu tu.

Kimanta amefanya ziara fupi katika wilaya ya Arumeru, baada ya maelekezo yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari John Pombe Magufuli dhidi ya tuhuma za ulimaji bangi katika wilaya hiyo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...