Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Baada ya kumalizika Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi hivi karibuni ulioongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Dkt. John Pombe Magufuli, na kipenga kupulizwa tayari kwa mbio za kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi kupitia Chama hicho, Wanachama wa Chama Hicho Mkoani Kagera wameonekana kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kuongoza nafasi katika nyadhifa za Udiwani na Ubunge katika maeneo yao.

Kufutia haki ya Kidemokrasia na Kikatiba kwa Mujibu wa Chama cha Mapinduzi, wanachama wengi wamejitokeza kuchukua fomu ikiwa ni siku ya kwanza, namiongoni mwao zikionekana sura mpya na wale waliomaliza muda wao katika kipindi cha kwanza cha awamu ya tano, na wengine wakiwa ni wale ambao waliwahi kuonekana wakati wa uchaguzi Mkuu 2015. 
Miongoni mwa waliofika katika ofisi hizo na kuchukua fom ni wakili msomi Allon Kabunga ambaye ni mwenyekiti wa chama cha mawakili wa kujitegemea kanda ya Kagera ambaye amesema kuwa licha ya kuwa yeye ni wakili laki pia ni mwanachama hai wa chama hicho hivyo baada ya kujipima ameona anatosha kuwatumikia wanabukoba mjini kupitia ubunge.

Mapema katika Ofisi za CCM Wilaya ya Bukoba na zile za Mkoa Kagera wameonekana wanahama kuvuta fomu za kuwania Ubunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini akiwemo Mbunge aliyemaliza wakati wake Dkt. Jasson Rweikiza, ambae nyuma yake wamefuata wanachama mbalimbali kutoka kada tofauti wakiwemo Vijana na Wazee wenye ari na morali, miongoni mwao ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kakangaga Muslim Ndg. Abdul Jalil Sheikh Mustafa, Mkufunzi wa Chuo cha Usafirishaji Taifa (NIT) Ndg Enock Mujwahuzi na wengine wengi.

Hali kama hiyo imejitokeza pia katika Ofisi za CCM Wilaya ya Bukoba Mjini ambapo mchuano unaonekana kuwa mkali baada ya wanachama zaidi ya 30 kujitokeza kwa wingi ikiwa ni siku ya kwanza, ikumbukwe kuwa Jimbo la Bukoba Mjini lipo chini ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) huku miongoni mwa waliojitokeza ni pamoja na Wakili Msomi Aaron Kabunga, Ndg. Kilwanila Kiiza aliyewahi kuwa Katibu wa Hospitali ya Rufaa Bukoba.
 Wakili Msomi Ndg. Aaron Kabunga kutoka Chama cha Mawakili nae kavuta fomu ya Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini kama anavyoonekana akikabidhiwa fomu yake.
 Ndg Inncoent Bashungwa akionekana kuchukua fomu ya kutetea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Karagwe, tayari kuomba ridhaa ya kupeperusha Bendera ya CCM kwa miaka Mingine mitano
 Kutoka kada ya Elimu anaonekana Mkuu wa Shule ya Kiislamu Kakangaga iliyopo Kigoma Ndg. Abdul Jalil Mustafa akipokea fomu ya Kuwania Ubunge Jimbo la Bukoba Vijijini.
 Kutoka kada ya Afya Ni Ndg. Kilwanila Kiiza aliyewahi kuwa Katibu wa Hospitali ya Rufaa Bukoba nae tayari kachukua fomu akiwania Ubunge wa Jimbo la Bukoba Mjini.
 Kwa kujiamini na ujasiri Mkubwa Ni Mkurugenzi wa Kituo cha Redio, Radio Vision ya Bukoba Ndg. Varelian Rugabaramu  kutoka sekta ya Habari akionesha Fomu yake ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Bukoba.
 Upande wa Vijana na wao hawapo Nyuma, Ndg. Joanfaith Kataraiya akipokea fomu yake atyari kwa kinyang'anyiro cha kuwania Uwakilishi wa Vijana Mkoani Kagera.
Wafanyabiashara nao ni kundi lililojitokeza kuwania Ubunge kama anavyoonekana Ndg. Audax Mwijage (Omujumba) akikabidhiwa fomu yake ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Bukoba.
Kwa Umakini Mkubwa anaonekana Bi Oliva Semunguruka akijaza fomu ya Kuwania Ubunge wa Viti Maalumu Mkoa Kagera, ambaye pia anatetea nafasi yake, yeye amejaza na kuikabidhi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...