WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa ametembelea Banda la Wakala wa Vipimo nchini (WMA) kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
Mhe. Bashungwa amesisitiza WMA kuendelea kufanya kazi kwa bidii ikiwa ni pamoja kuhakikisha vipimo vyote nchini vinakuwa sahihi ili Tanzania iweze kufikia Uchumi wa Viwanda ambapo tayari tumefikia Uchumi wa Kati kwa mwaka huu wa 2020.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa akinyanyua jiwe la mzani katika Maonesho ya viwanja vya Julius Nyerere maarufu kama Sabasaba, barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...