MBUNGE wa Viti Maalum anaewakilisha Vijana (CCM), Mariam Ditopile ampongeza Rais John Magufuli kwa kuiwezesha Tanzania kupaa na kufikia uchumi wa kati kabla ya Mwaka 2025.

Malengo ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli iliweka malengo ya kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 lakini badala ya kutumia miaka 10 kufikia malengo hayo imetumia miaka mitano pekee.

Akizungumza jijini Dodoma baada ya taarifa hiyo ya Benki ya Dunia kuitangaza Tanzania kufikia uchumi wa kati, Mbunge Ditopile amesema mafanikio yote hayo yametokana na kasi ya utendaji kazi wa serikali unaosimamiwa na Rais mwenyewe.

Amesema ndani ya miaka mitano hii ya kwanza, Rais Magufuli amefanya kazi kubwa ya kuimarisha amani nchini pamoja na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo imepelekea ukuaji wa uchumi nchini.

" Sasa ni wazi Dunia nzima inamuelewa Rais Magufuli na inajua Tanzania imebarikiwa kuwa na kiongozi na mwenye maono ya kipekee. Kama malengo yalikua ndani ya miaka 10 tufikie uchumi wa kati badala yake tumetumia miaka mitano pekee maana yake hii watanzania tunapaswa kumuongezea Rais Magufuli miaka hii mitano mingine ili atufanyie makubwa zaidi.

Ndani ya miaka mitano Rais Magufuli ametunyanyua kutoka kuwa Nchi maskini na kuwa miongoni mwa Nchi 50 zenye uchumi wa kati, ni wazi kwa mafanikio haya Rais wetu atapita kwa kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu ujao hapo Oktoba, " Amesema Mbunge Ditopile.

Amesema mafanikio yote haya yanatokana na usimamizi mzuri wa sera, utendaji kazi uliotukuka na uzalendo na kwamba watanzania wana kila sababu ya kugombea kifua mbele kujivunia kumpata Rais mchapakazi mwenye kuyaishi maono yake.

" Mafanikio haya yanatokana na ujenzi wa Nchi, miundombinu inayojengwa nchi nzima imewafikia watanzania wengi kujikwamua kiuchumi kwa sababu kupitia miradi hii wapo watanzania wengi wamepata ajira, wengine wamefanya biashara.

Umeme Vijijini (REA) pia umechangia ukuaji wa uchumi, lakini Sera ya elimu bila malipo ambayo Rais wetu anawalipia wanafunzi ada kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha nne zaidi ya Bilioni 20 kila mwezi kumepunguza matumizi ya fedha kwa watanzania wengi, zote hizi ni sifa kwa Rais Magufuli, " Amesema Ditopile.

Mbunge huyo amewataka vijana nchini kutembea kifua mbele kujivunia kazi inayofanywa na serikali na kuwa mabalozi wa kuyasema yale makubwa yote yanayofanywa na Rais na kuhakikisha wanampigia kura nyingi za ndio ili aweze kuendelea na kipindi chake cha pili.

" Watanzania wenzangu kama ndani ya miaka mitano tu tumefikia uchumi wa kati, vipi kama atamalizia miaka mingine mitano? Maana yake tutakua tumepiga hatua kubwa sana kiuchumi na kuyafikia mataifa makubwa ulimwenguni," Amesema Ditopile.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...