Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya
Kitaifa ya Maandalizi ya Mazishi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ,
Benjamin William Mkapa wakati alipokagua maandalizi ya Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es salaam Julai 25, 2020 ambapo kutafanyika Ibada ya
kumwombea marehemu na kuaga mwili kitaifa kuanzia kesho. (Picha na
ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi
Seif Ali Iddi ( wa pili kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, Jenista Mhagama (kushoto) wakati walipokagua Maandalizi ya
Mazishi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa kwenye
Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Julai 25, 2020 ambapo kutafanyika
Ibada ya kumwombea marehemu na kuaga mwili kitaifa kuanzia kesho. Wa
nne kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohammed Abood na kulia ni Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi John Kijazi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...