Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro – Mathayo Masele akikata
utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa tawi la Benki ya NMB Malinyi . Wengine
katika picha kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mkuu wa Kitengo cha Mikopo
waa NMB – Demetus Kaguna, Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na
Biashara wa NMB – Salie Mlay – Meneja wa NMB Kanda ya Mashariki –
Dismas Prosper na Meneja wa Tawi la Malinyi – Ipyana Mwakatobe.
Mkuu
wa Wilaya ya Malinyi – Mathayo Masele na Kaimu Afisa Mkuu wa wateja
Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB Salie Mlay wakipiga makofi baada ya
kufunguliwa rasmi kwa tawi la Benki ya NMB Malinyi

…………………………………………………………..
Benki ya NMB imeendelea kupanua wigo wake kwa kufungua tawi ‘NMB
Malinyi’ katika wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro. Ufunguzi wa tawi
hili umeleta ahuweni kwa wakazi waliokuwa wanasafiri umbali wa kilomita
160 kwenda mji wa Ifakara Wilayani Kilombero kupata huduma za kibenki.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo, Mkuu wa
Wilaya ya Malinyi – Mathayo Masele amesema tawi hilo limekuwa
likisubiriwa kwa hamu sana kwani NMB ndio taasisi ya kwanza kufungua
tawi ambapo anaamini litachochea ukuaji wa uchumi na maendeleo katika
eneo hilo kutokana na kuongezeka kwa kasi ya uzalishaji wa mazao ya
kilimo, mifugo pamoja na uchimbaji wa madini ya dhahabu ambayo
yamegunduliwa hivi karibuni.
Masele alisema kuwa Benki hiyo licha ya kukuza uchumi pia
itawapunguzia gharama wafanyabishara, na Taasisi ambazo zilikuwa
zikitumia gharama kubwa kwaajili ya kusafirisha fedha kwa usalama zaidi
Mwakilishi wa Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Salie
Mlay, alisema moja ya kichocheo kikubwa cha kufungua tawi hilo ni
kuwasaidia wakulima na wafugaji waweze kupata mikopo pamoja na elimu ya
ushirika utakaowapa tija kwa kutumia mfuko wa NMB Foundation.
Sambamba na uzinduzi huo, NMB imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi
vikiwemoa mabati, kofia, misumari na mbao kwaajili yakukamilisha
uwezekaji vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Nawigo iliyopo
Malinyi. Ikiwa ni sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...