Na mwandishi wetu, Nanyumbu

KAMPENI ya kuhamasisha wanachi kutumia nishati ya umeme inayoratibiwa na idara ya masoko ya SHIRIKA la umeme Tanzania TANESCO makao makuu imetua mkoani Mtwara.

Maafisa wa TANESCO wakiongozana na Meneja wa TANESCO wilaya ya Masasi mkoani Mtwara, Mhandisi Sidala Maeda wametembela vijiji kadhaa vikiwemo vya Liputi, Raha leo na Namyomyo na baadaye timu iliungana na Meneja wa Shirika hilo wilaya ya Nanyumbu Mhandisi Peter Mwaimu na kufika vijiji vya Tuungane, Mtalikachao

Timu hiyo ikiwa kwenye vijiji hivyo ilifanya mikutano na wananchi na kutoa elimu kuhusu matumizi bora na sahihi ya umeme, faida itokanayo na nishati ya umeme ikiwa ni pamoja na kuwahamishwa wanachi kutumia nishati hiyo kujiletea maendeleo.

“Lakini pia tumetoa elimu ya jinsi ya kuwaunganishia umeme wana vijiji katika wilaya hizo kwa gharama nafuu ya Shilingi elfu ishirini na saba tu ( 27,000/=).” Alisema Mhandisi Maeda.

Alisema  wananchi wote wataunganishiwa  umeme kwa wakati hivyo basi aliwasisitiza kufanya  mtandao (wire ring)  ndani ya nyumba zao kwa kuwatumia wakandarasi waliosajiliwa na kuepuka vishoka.

Wilaya ya masasi pekee ina jumla ya vijiji 67 kati ya vijiji hivyo 43 tayari vineshanufaika kwa kuwashiwa umeme.

Kwa upande wake Meneja wa TANESCO wilaya ya Nanyumbu Bw. Peter Mwaimu licha ya kuwahamasisha wananchi kutumia nishati ya umeme lakini pia amewaelimisha kuhusu matumizi salama ya umeme ili kuepuka athari za matumizi umeme yasiyozingatia usalama.

Afisa uhusiano na huduma kwa wateja mkoa wa Mtwara bw Jumanne Nkunguu akielezea wananchi wa Liputi kuhusu ulinzi wa miundo mbinu na matumizi bora ya umeme
Afisa Masoko TANESCO makao makuu Bi. Jennifer Mgendi (kulia) akielezea wananchi wa Tuungane kifaa cha UMETA au umeme tayari ambacho hutumika badala ya wiring, wale ambao hawatafanya wiring watumie kifaa hicho
Wananchi wa Mtalikachao wakimsikiliza meneja wa TANESCO wilaya ya Nanyumbu (hayupo pichani) Bw. Peter Mwaimu akiwaeleza jinsi miradi ya umeme vijijini inavyoendelea na kuwaelezea usalama wa umeme na athari zake

Afisa masoko TANESCO makao makuu Bi. Jennifer Mgendi akielezea taratibu za kuunganishiwa umeme kwa kwa  gharama nafuu ya Shilingi 27,000/= tuu na kuwashauri wananchi kutumia wakandarasi waliosajiliwa katika Kijiji Cha Raha leo wilaya ya Masasi mkoani Mtwara

 Meneja wa TANESCO Wilaya ya Masasi mkoani  Mtwara, Mhandisi Sidala Maeda akizungumza na wanakijiji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...