Na Abdullatif Yunus Michuzi Tv.
Benki
ya CRDB imeendelea kutoa Semina Wezeshi kwa Mawakala wake Mkoani Kagera
Juu ya namna ya kuboresha huduma zitolewazo na Benki hiyo kitengo Cha
Mawakala, katika Ukumbi wa E.L.C.T Bukoba Agosti 19,2020.
Semina
hiyo iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco
Gaguti, imehudhuliwa na Mawakala zaidi ya 100 kutoka katika Matawi ya
Wilaya za Bukoba mjini, Muleba & Rwamishenye ikiwa ni muendelezo wa
semina hizo kwa kanda ya ziwa na maeneo mengine ya Nchini.
Tangu
kuanzishwa kwa huduma ya Mawakala mnamo Mwaka 2013, kwa sasa CRDB ina
mawakala zaidi ya 16,000 waliotapakaa Tanzania nzima, na ina mawakala
zaidi ya 400 katika Mkoa wa Kagera, hii inafanya CRDB kuwa na mawakala
wengi kuliko Benki yeyote Nchini ikiwa imetengeneza takribani zaidi ya
ajira elfu 20.
Mawakala
wa CRDB wamesaidia kuongeza huduma za kibenki kwa kuongeza muda wa
wateja kufanya miamala ambapo baadhi ya mawakala wanatoa huduma kwa
masaa 24.
Semina
ya mawakala imelenga pia kuwakumbusha mawakala kufuata taratibu na
kanuni zote za kifedha kama zinavyosimamiwa na Benki kuu. Wakala hao
wamepewa Elimu kuhusiana na elimu ya utakatishaji Fedha. Sambamba na
Hilo CRDB imetoa elimu ya ujasiliamali na njia nzuri zaidi ya kuhudumia
wateja wa benki, pamoja na kusaidia kuongeza wateja ili wananchi
waendelee kufurahia huduma zetu, pia CRDB wamewakumbusha huku mawakala
hao wakikumbushwa Juu ya kuhudumia wateja wao kwa uadilifu mkubwa na
kuhakikisha wanatunza siri za wateja kwa uaminifu mkubwa
Meneja
wa CRDB Tawi la Bukoba, Synden Bakari akizungumza kabla kumkaribisha
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti
kuzungumza na Mawakala wa Mkoa Kagera.
Meneja wa CRDB Tawi la Mulebba, Mr. Mbaga akisistiza na kutolea ufafanuzi Jambo wakati wa maswali na majibu ndani ya Ukumbi wa ELCT Bukoba.







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...