Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Klolo amewaagiza wakandarasi wote wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza kuzingatia na kutekeleza maelekezo yote yanayotolewa katika vikao kazi vya kila mwezi ambavyo vinafanyika katika maeneo ya miradi ili waweze kukamilisha ujenzi wa miundombinu na kuunganishia wananchi umeme katika muda wa nyongeza waliopewa.

Wakili Kalolo alitoa agizo hilo tarehe 05/08/2020 wakati Bodi yake ilipofanya uk aguzi wa utekelezaji wa Mradi huo katika Wilaya ya Nyang’alwe na kufanya kikao cha pamoja kati ya Bodi ya Nishati Vijijini, watendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), TANESCO na mkandarasi Kampuni ya White City.
Wakili Kalolo alisema kuwa hawataongeza tena muda na kusisitiza wakandarasi wote wakamilishe kazi mwezi huu na watakaoshindwa watachukuliwa hatua kwa kuzingatia mikataba yao ya kazi.

Akizungumza suala hilo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Ufundi wa REA Mhandisi Jones Olotu alisema wakandarasi wanachelewa kukamilisha kazi kwa wakati uliopangwa kutokana na kutokuzingatia maelekezo yanayotolewa katika vikao kazi. “Wakandarasi wazingatie maelekezo ya vikao kazi (site meeting) kukaidi maelekezo kunasababisha kazi kuchelewa kukamilika jambo linalopelekea wakandarasi kuomba muda wa nyongeza” alisisitiza.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya White ambayo inatekeleza Mradi huo katika Mkoa wa Geita, Nuhu Mringo alisema kuwa walichelewa kukamilisha kazi kutokana na kukwama kwa vifaa vya ujenzi walivyoagiza nchini China kutokana na janga la ugonjwa wa Corona. Hata hivyo alisema kuwa vifaa hivyo vimeshawasili na kuahidi kumaliza kazi katika muda wa nyongeza aliopewa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...