Team ya Brela ikiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha Bakari Ally Mketo wa pili kutoka kushoto wakiwa tayari Banadri kutoa huduma
Afisa kutoka Brella Bi Sada Kilabula kulia akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda lao kwenye maonyesho ya nane nane mkoani Lindi
WAKALA wa  usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeshiriki maonyesho ya wakylima nane nane kwenye mikoa ya Simiyu na Lindi ili kuweza kuwafikia zaidi wananchi wake katika utoaji wa elimu ya kurasimisha biashara na huduma zinazotolewa na wakala huo.

BRELA ni Taasisi  iliyopo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara ambayo jukumu la taasisi ni kusajili majina ya Biashara, makampuni, nembo za huduma na biashara, Hataza, Utoaji wa leseni za Biashara daraja A na Leseni za Viwanda.

Katika Mkoa wa Lindi kwenye Maonyesho hayo wakala huo uliwakilishwa na Mkurugenzi wa Utawala na fedha Bakari Mketo ambaye alibainisha kwamba lengo kuu la kushiriki katika maonesho hayo ni kuhakikisha wananchi wote wanapata huduma na utatuzi wa changamoto wanazokutana nazo wakati wa kufanya sajili mbalimbali za BRELA papo kwa papo.

Pamoja na yote amewataka wakulima na wadau mbalimbali kuweza kurasimisha biashara zao ili kutambulika na kuweza kuufikia Uchumi wa kati.

Pia ameeleza kwamba dhumuni la kushiriki maonesho ni kuwasogezea wananchi wa lindi huduma kwa ukaribu na kuendelea kutoa mafunzo juu ya utumiaji wa mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao.

Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanatembelea katika banda lao lililopo katika viwanja vya Ngongo ili kuweza kupata huduma za sajili papo kwa papo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...