NA MWAMVUA MWINYI,PWANI
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM )mkoani Pwani kimewaasa baadhi ya wanachama wake
kuondoa makundi na kuacha kuwekeana chuki badala yake waungane kuwa
wamoja na kushikana baada ya uchaguzi wa ndani kukamilika .
Kimeeleza
,kwasasa hatua mbalimbali zitaendelea na vikao vya maamuzi ya kuteua
wagombea watakaopeperusha bendera katika uchaguzi mkuu unaokuja hivyo
haina budi kuwa watulivu na upendo .
Akielezea
mchakato wa uchaguzi walivyojipanga baada ya hatua za awali za chama
kukamilika ,katibu wa CCM mkoani Pwani ,Anastazia Amas alisema mkoa
umejidhatiti kushinda kwa kishindo chaguzi nafasi ya Urais,wabunge na
madiwani.
Alieleza ,haina ubishi mchakato wa kura za maoni umeenda kidemokrasi hivyo kilichobakia sasa ni kuwa wamoja .
"Chuki
na visasi kwasasa havina nafasi ,wanachama wawe pamoja ,sio kama wapo
wanaowekea chuki bali katika uchaguzi wowote hakukosekana makundi
lakini sasa vitendo hivyo vifikie kikomo:"alielezea Amas .
Amas
alifafanua, hatua za uchukuaji wa fomu ulikuwa wa kidemokrasia
,wanachama walijitokeza kwa wingi kuanzia ubunge wa majimbo Tisa na
ubunge viti maalum,madiwani.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...