Na Amiri Kilagalila,Njombe
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimelazimika kuahirisha zoezi la mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama hicho Mh,Tundu Lisu,kuendelea kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo taratibu za kujaza fomu kwa usahihi.
Uamuzi huo umetangazwa na mgombea wa Urais Tundu Lisu wakati wa ziara yake ya mwisho hii leo mjini Njombe huku akiomba radhi kwa wananchi wa mikoa iliyokuwa imesalia.
“Ratiba
yetu ya mwanzo ilikuwa inasema baada ya mkoa wa Njombe, tungeenda
Songea,Mtwara,Lindi halafu siku ya tarehe 21 Tungerudi Dar Es Salaam ili
tarehe 22 twende Dodoma kuwasilisha fomu za uteuzi wa Rais na Makamu wa
Rais”alisema Lisu
“Haitawezekana tena kwenda hiyo mikoa mitatu kwasababu ambazo zipo juu ya uwezo wetu,hizi fomu ni nyingi zinatakiwa kujazwa kwa usahihi,mikoa yote ambayo tumepita kazi mmefanya vizuri sana na kuna kazi ambayo katibu mkuu wetu anatakiwa aifanye kwa usahihi na kazi hiyo isipofanyika kwa usahihi katika sehemu zote nilizozisema hatuna mgombea na kama hatuna mgombea hatutakuwa na kampeni”aliongeza Lisu
Kwa upande wake mgombea wa Ubunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (SUGU) aliyeongozana na viongozi wa kitaifa mkoani Njombe amewaomba wananchi wa jimbo la Njombe kuungana kwa sasa ili kufanikisha ushindi wa Chama hicho na kupata majimbo mengi.
“Nipo Njombe kwasababi ni kanda ya Nyasa na sisi kanda ya nyasa tunataka tuhakikishe tunakuwa na majimbo mengi zaidi na kura nyingi kwa ajili ya Urais ili kuing’oa serikali ya Chama cha Mapinduzi”alisema Sugu
Naye
mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Njombe Rose Mayemba kwa niaba ya wananchi
wa mkoa wa Njombe amemshukuru kiongozi huyo kwa kufika mkoani Njombe
kwani wamefurahishwa na ujio wake.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...