Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv
Uongozi wa Klabu ya Dodoma Jiji umeweka wazi kikosi cha wachezaji 26 kitakachoshiriki Ligi kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2020/21.
Dodoma Jiji, imewatangaza wachezaji hao leo hii na kuwajulisha mashabiki wake kuwa kikosi chao kimekamilisha usajili wake kwa ajili ya kuimarisha timu hiyo kuelekea msimu ujao.
Wachezaji waliotangazwa kuwepo katika kikosi hicho ni pamoja na magolikipa watatu Hussein Masalanga, Emmanuel Mseja na Aron Kalambo.
Wengine ni mabeki, Anderson Solomon, Abubakari Ngalema, Ibrahim Ngecha, Mbwana Kibacha, Hassan Kapona, George Wawa, Jukumu Kibanda, Augustino Ngata na Justine Omary.
Kwa upande wa Viungo ni Rajab Seif, Steven Mganga, Jamal Mtegeta, Omar Kanyoro, Deus Kigawa, Salmin Hoza, Cleophace Mkandala, Peter Mapunda na Dickson Ambundo.
Washambuliaji Anuary Jabir, Khamis Mcha, Santos Thomas, Seif Karihe na Michael Chinedu.
Timu iyo kwa sasa ipo katika maandalizi ya msimu mpya unaoatarajia kuanza Septemba 06 baada ya kupanda ligi kuu msimu wa 2020/21
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...