Nally ni msanii wa kike anayechipukia kwa kasi katika medani ya Bongoflava. Alianza kuimba tangu 2016, lakini hakujiamini sana, hivyo akaamua kwanza ajikite kwenye tasnia kama Video Vixen na Dansa.
Pia alikuwa anasaidia kujazia sauti za nyuma [background vocals] kwenye nyimbo za wasanii katika studio mbalimbali.
Nally pia aliigiza kwenye tamthilia kadhaa [Arawa, Chaguo Langu]
Mwaka 2018 akaamua kujitosa kimoja kwenye muziki.
'Nyang'anyang'a' na 'Liar', singo zake za mwanzo zilionyesha matumaini.
Mwaka 2019 mwanzoni akamuomba Master T - Taji Liundi asimamie kazi zake.
Baada ya kukubaliwa, haraka akarekodi EP ya kwanza ambayo ina singo kuu 'Tetere' collabo na Msanii Barnaba Classic, 'Huku' na mwandishi wake Passo, 'Rafiki' na Nitho P msanii wa Dodoma pamoja na wimbo 'Pampara'.
Hata hivyo Nally amerekodi wimbo wa 'Teleza' akimshirikisha msanii wa Dancehall kutoka Jamaica anaitwa Squeel.
Licha ya hili msaani huyu amerudia kuimba wimbo wa Mama Patricia Hillary msanii mahiri wa muziki wa Taarabu ambapo mwenye wimbo aliridhia kurudiwa kwa wimbo wake maarufu 'Njiwa Peleka Salamu' ambao umepigwa kwa midundo ya kisasa.
July 1, Nally alitoa singo na video bunifu ya wimbo 'My' ambayo imefanya vizuri zaidi na kumsogeza mbele kitasnia.
MSANII HADI MENEJA
Nally anasimamia wasanii mbalimbali katika mradi ambao anausimamia yeye mwenyewe unaitwa 'Pamoja Project'
Pamoja Project:
Umetokana na malengo ya Uongozi wa lebo yake ya Masters Work kutekeleza azma ya kukuza vipaji.
Pamoja Project inatafuta na kushirikisha kikamilifu wasanii wachanga kurekodi kwa pamoja ngoma bora. Inajenga umoja, inakuza vipaji vyao na kuleta mshikamano Pamoja Project inasaidia wasanii kushirikiana kikazi, haswa kwenye kusukuma kazi, promotion na kutafuta fursa za kujiendeleza.
Meneja wa Project ni Nally, wasanii baadhi ni kama Darbelong, Sumatoto, Chankybella na Passo. Mtayarishaji Mkuu ni Producer Perfect na
Mkurugenzi Muongozaji ni Taji Liundi.
Tayari Pamoja Project imesharekodi nyimbo tatu Nsomeshe
Twende na Koloni ambao utazinduliwa Novemba 2020.
'Nsomeshe' na 'Twende' zilitangulia akiwa na wasanii Darbelong na kundi la Yeamen. Inatarajiwa kwamba mradi huu wa kipekee utabadilisha mwenendo wa tasnia ya Bongoflava kwa kusisitiza.
Ubora wa production/utayarishaji wa nyimbo hadi video
Umuhimu wa kukuza vipaji, Umuhimu wa kushirikiana ni kuweka nguvu ya pamoja kuingia sokoni.
Nally ataimarika kama msanii na pia kama Kiongozi mwenye uelewa mkubwa wa Tasnia.
Kuelekea Chaguzi Kuu 2020, Nally amerekodi wimbo wa Hamasa kwa Wanachama wa Chama cha Mapinduzi unaoitwa ''Mi5 Tena - CCM''.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...