JESHI la Polisi Nchini limesema limejipanga kikamilifu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na kwamba yeyote atakayejaribu kuvuruga amani ya nchi atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Akizungumza wakati akiwa mkoani Pwani kwenye ziara maalum ya ukaguzi Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi CP Liberatus Sabas amesema kuwa, Jeshi la Polisi limeendelea kuimarisha mazoezi mbalimbali kwa askari wake.
Hata hivyo, kamishna Sabas amesema kuwa, hadi sasa kuna operesheni maalum inayoendelea katika mikoa ya Pwani, Morogoro na Iringa, operesheni ambayo itasaidia kupunguza uhalifu.
Wakati huo huo Kamishna Sabas amewataka wananchi kuendelea kutii sheria bila kushurutishwa huku wakiwafichua watu wanaojihusisha na uhalifu kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya dola.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...