Inspekta Jenerali wa jeshi la Polisi Simon Sirro akizungumza leo katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre (JNICC) jijini Dar es salaam.
Na Mwandishi wetu, Globu ya Jamii
ASKALI wa jeshi la polisi nchini wamejiandaa vizuri kusimamia uchaguzi uliopo mbele yetu kwa kubaini makosa hata kabla hayajatokea na kumchukua hatua ikiwa pamoja na kuandaa mashtaka na kuwapeleka watuhumiwa mahakamani kwa mujibu wa sheria.
Hayo yamesemwa na Inspekta Jenerali wa jeshi la Polisi Simon Sirro wakati akitoa mada leo tarehe 19.08.2020 kuhusu ulinzi na usalama katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Julius Nyerere Convention Centre (JNICC) jijini Dar es salaam. Amesema kuwa hali ya uhalifu nchini imepungua kwa kiasi kikubwa.
Hat hivyo Sirro amesema kuwa mikakati iliyopo ni kuhakikisha amani na usalama vinatawala wakati wote wa kuchukua fomu kwa Wagombea, urejeshaji wa fomu, kampeni, upigaji kura, kuhesabu kura, kutangaza matokeo na kusherehekea ushindi.
Amesema kuwa makosa ambayo yamekuwa yanajitokeza ni makosa ya mitandao ya kijamii kama Jamii forum, Facebook, Instagram, twitter, Blogs na Whatsapp nayo yatadhibitiwa.
Aidha wakati akitoa mada Inspekta Jenerali wa Polisi Sirro amesema kuwa amani ni muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu hivyo viongozi wa vyama vya siasa kufuata sheria za uchaguzi na tume ya uchaguzi kuweka taratibu zote za uchaguzi mapema ili kuondoa mapungufu yanayoweza kuleta taharuki.
Alisema viongozi wa siasa watapita lakini nchi itabaki kama nchi, pia hasira huondoa busara na ukitaka kufa tafuta njia nyingine ya kufa na si kutumia siasa.
"Tumejipanga vizuri kutoa ulinzi kwa wagombea na wagombea wenza kwa wagombea wote watakaopitishwa na Tume ya Uchaguzi." Ameitimisha Sirro.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...