Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akipokea msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram)
kutoka kwa Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii
ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for
tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya watoto wanaotibiwa
katika Taasisi hiyo. Thamani ya mashine hiyo ni milioni 17.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpulizia kisafisha
mikono (hand sanitizer ) Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke
Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany
Society for tropical pediatrics) mara baada ya kumkabidhi msaada wa
mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) kwa watoto
wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Thamani ya mashine hiyo ni milioni 17.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi
akizungumza na wazazi kuhusu umuhimu wa kufanya kipimo cha kuchunguza
moyo wa mtoto aliyepo tumboni kwa wamama wajawazito (Fetal Cardiograph).
Wazazi hao walifika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwaleta
watoto wanaotibiwa Jkci kliniki.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...