Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele (kushoto) akiwa na Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini,Patrobas Katambi (katikati) na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Abubakari Gulam mara baada ya Patrobas Katambi kurudisha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumanne Agosti 25,2020.
**
====== ====== ======
Na Victoria Robert - Michuzi blog.
Mgombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Patrobas Katambi amerudisha fomu kwa msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi.
Katambi amekabidhi fomu kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumanne Agosti 25 akiwa ameambatana na viongozi na wanachama wa CCM akiwemo Mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo hilo Stephen Masele.
Akizungumza baada ya kukabidhi fomu, Katambi ameahidi kufanya kampeni kwa amani na utulivu pamoja na kuwatumikia wananchi wa Shinyanga kwa kuzingatia makundi yote katika jamii ili kuwainua kiuchumi na kijamii.
Naye Masele amezitaka timu zote ambazo zilizokuwa zimejengwa na watia nia wa chama hicho kuzivunja na badala yake kumuunga mkono mgombea wa chama hicho huku akidai kuwa hataondoka katika chama chake na atakuwa bega kwa bega na Katambi katika kuleta ushindi kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi Mkuu 2020.
Mgombea nafasi ya Ubunge katika jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Patrobas Katambi akirudisha fomu kwa msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi leo Jumanne Agosti 25,2020.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele (kulia) na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Abubakari Gulam (katikati) wakiwa na Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini, Patrobas Katambi wakati akirudisha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumanne Agosti 25,2020.
Viongozi na wanachama wa CCM wakimsindikiza Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini,Patrobas Katambi kurudisha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini.
Viongozi na wanachama wa CCM wakimsindikiza Mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini,Patrobas Katambi kurudisha fomu ya kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...