Na Shukrani Kawogo, Njombe.

Baadhi ya wazawa wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ambao wameunda kikundi cha Whatsapp chenye watu 194 wametoa msaada wa magunia 70 ya mahindi pamoja na debe 11 za maharage katika shule ya mahitaji maalum iluyopo wilayani humo katika kata ya Mundindi.

Wakikabidhi chakula hicho baadhi  ya wanakikundi hao wamesema kuwa Katika mradi wa shamba kikundi kilikodi shamba la ekari nane (8) ambazo kati ya hizo ekari saba zilikuwa za mahindi na ekari moja ilikuwa ya maharage. 

Waliongeza kuwa mchakato mzima umegharimu kiasi vha shilingi ml. 4,238,000 ambapo mchanganuo wake ni kuanzia kukodi shamba kufyeka miti,kulima, kupanda, kununua mbegu kupalilia na shughuli nyingine hadi kuvuna,kupiga na kufikisha mazao shuleni.

Akipokea msaada huo mkuu wa shule hiyo Amos Mtitu amekishukuru kikundi hicho kwa msaada huo na kuwaomba waendelee kuwa na moyo wa kusaidia watu wenye uhitaji.

Kikundi hicho kina miaka sita tangu kuanzishwa kwake ambapo mpaka sasa wameshatoa msaada katika sekta mbalimbali ikiwemo afya na elimu na kinaongozwa na Yombayomba Yombayomba pamoja na Mwl. Benjamin Mtweve.

Hata hivyo kikundi hicho kinaendelea kuwakaribisha watu wote wenye mapenzi mema na Ludewa kujiunga nao ili kuunga mkono harakati za kutoa michango mbalimbali kwa jamii ili kukuza maendeleo.
 Mmoja wa wanakikundi  cha whatsapp cha wazawa wa Ludewa Sabinus Haule (wakwanza kulia) akimkabidhi mahindi mkuu wa shule ya mahitaji maalum Amos Mtitu ( wakwanza kushoto)
 Wanakikundi cha wazawa wa Ludewa wakiongea na baadhi ya wanafunzi Katika shule ya mahitaji maalum
 Magunia 70 ya mahindi   na debe 11 za maharage waliyokabidhiwa uongozi wa shule ya mahitaji maalum iliyopo Mundindi wilayani Ludewa kutoka kwa wanakikundi cha Whatsapp cha wazawa wa Ludewa
 Baadhi ya madiwani waliopita kwenye kura za maoni ambao walijumuika na wanakikundi hao, kutoka kushoto ni Edward Haule( Diwani kata ya Ibumi na mwenyekiti wa Halmashauri aliyemaliza muda wake) , Wice Mgina (Diwani wa kata ya Mundindi) pamoja na Vasco Mgimba (Diwani kata ya Ludende)
 Baadhi ya wanakikundi wakiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji wa serikali pamoja na walimu wa shule ya mahitaji maalum Mundindi
 Baadhi ya wanafunzi wanasoma shule ya mahitaji maalum Mundindi wakiwa na walimu wao kwa ajili ya kupokea msaada wa mahindi na  maharage kutoka kwa wanakikundi cha Whatsapp cha wazawa wa Ludewa
 Vasco Mgimba ambaye ni Diwani aliyeshinda kura za maoni CCM kata ya Ludende ( wakwanza kulia) skifurahi na watoto wenye mahitaji maalum Katika shule ya Mundindi
Mkuu wa shule ya mahitaji maalum Mundindi, Amos Mtitu akisoma barua ya shukrani kwa wanakikundi cha Whatsapp cha wazawa wa Ludewa baada ya kutoa msaada wa gunia 70 za mahindi na debe 11 za maharage.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...