Na Said Mwishehe,Michuzi TV

MAMLAKA  ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo imefungua rasmi kliniki ya methadone katika Hospitali ya Tumbi, Kibaha inayoa tiba ya uraibu wa dawa za kulevya.

Taarifa ya Mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari imesema Kliniki hiyo imeanza kutoa huduma  leo Agosti 27,2020  kwa waraibu wa dawa za kulevya ikiwa pamoja na kunywa dawa  ya Methadone.

Imefafanuliwa kuwa sambamba na tiba ya uraibu wa dawa za kulevya Kliniki hiyo itatoa na huduma za matibabu ya magonjwa mengine kama UKIMWI ,TB, Malaria na magonjwa ya akili.

"Kliniki hii ni ya tisa zikiwemo Muhimbili, Temeke,Mwananyamala ,Mbeya,Mwanza, Tanga,Dodoma na Bagamoyo ambazo pia zinatoa  tiba hiyo ya uraibu wa dawa za kulevya ambapo takribani waathirika 8000 wanapata huduma hiyo kila siku,"imesema taarifa ya Mamlaka hiyo kupitia Kitengo chake cha Mawasiliano.

Aidha Mamlaka hiyo inawahimiza wananchi kutowanyanyapaa waathirika wa dawa za kulevya na badala yake wawasaidie kuwapeleka kwenye vituo vya  huduma za afya ili wapatiwe tiba ya uraibu wa dawa za kulevya na hatimaye wawe raia wema watakaoshiriki kikamilifu katika ujenzi wa maendeleo ya Taifa.
 Mraibu wa dawa za kulevya  akinywa dawa ya Methadone kwenye dirisha la dawa.
 Waraibu wakisubilia kupata huduma kwenye Kliniki hiyo ambayo imeanza kutoa huduma leo katika Hospitali ya Tumbi ,Kibaha
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...