Na Said Mwishehe, Michuzi TV
CHAMA cha Wafanyakazi wa Madereva Tanzania(TADWU) kimesema kimetoa pongezi kwa Rais John Magufuli kwa namna alivyosimama imara katika mapambano dhidi ya Corona jambo ambalo lilisaidia hata huduma za usafiri nchini kuendelea bila kikwazo cha aina yoyote.
Akizungumza leo na waandishi wa habari katika Kituo cha Mabasi ya Mikoani Ubungo jijini Dar es Salaam Majura Kafumu amesema sekta ya usafirishaji ni sekta mama na imeshikilia uchumi wa nchi.
"Tunatoa pongezi kwa Rais Dk. Magufuli kwa jitihada ambazo amezifanya na leo tunaona maendeleo yaliyopo, natoa shukrani kwa namna ambavyo alitupa moyo wa uvumilivu kwenye jagnga la Corona ambalo lilikuwa limeikumba dunia.
Ameongeza na wao kama sehemu ya usafirishaji hawakukata tamaa,waliendelea kubeba abiria na kwa madereva wa malori nao waliendelea na safari zao katika nchi mbalimbali ambazo nazo zilikuwa na vikwazo kutokana na uwepo wa Corona.
Amesisitiza Rais Magufuli aliwahamasisha watanzania kufanya maombi kumuomba Mungu na hakika amejibu maombi." Tunamshukuru Mungu kwani hatukuathirika kwa kiwango ambacho watu walitegemea."
Kuhusu Chama hicho , Kafumu amesema kuna baadhi ya changamoto zinazokabili ikiwemo ya kanuni za adhabu kwa madereva ambayo tayari imeshasainiwa.Hata hivyo amesema kuna mazungumzo yanaendelea kuondoa changamoto hiyo.
"Tumeshakaa kikao na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kumuelezea changamoto hii ya kanuni ya adhabu kwa madereva ambayo kimsingi ni ya uonevu kwa upande wetu.
"Tumekuwa na mamlaka mbili ambazo zinasimamia usalama wa barabarani na hapo nako kuna mkanganyiko hapa.Hivyo tutakuwa na mazungumzo siku za karibuni,"amesema na kuongeza "haiwezekani hata abiria asipofunga mkanda adhabu ije kwa dereva ambaye yuko mbele anaendesha gari.
Hata hivyo amesema Chama hicho kina mamlaka kamili ya kutetea maslahi ya madereva nchini na ndio maana kimeamua kufuata utaratibu unaolekeweka kutafuta ufumbuzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...