Na Leandra Gabriel, Michuzi

LICHA ya baadhi ya maeneo kuwa hatarishi na kuogofya baadhi ya watu wamekuwa wakitembelea na kutalii, lakini baadhi ya maeneo yamepigwa kufuli kwa kutoruhusu watu kutembelea ili kulinda usalama wa raia wake, baadhi ni haya hapa;

1. Area 51, Marekani

Ni eneo la uwanja wa mazoezi ya kijeshi na lilizuia umma kutolitembelea kwa miongo kadhaa, linaelezwa kuwa no kituo cha siri cha kijeshi katika jangwa la Nevada na wengi wanaamini eneo hilo limetengwa kwa ajili ya mazoezi ya kijeshi na lipo chini ya ulinzi mkali siku zote. 



2. Kisiwa cha Heard, Australia

Kinafahamika zaidi kama kisiwa cha mlipuko au uwanja wa barafu, kinapatikana kati ya Madagascar na Antarctica, kisiwa hiki ni makazi ya wanyama mbalimbali  wa baharini.

Zuio la kutembelea kisiwa hicho kwa mara ya kwanza ilikuwa ni mwaka 2000 na hiyo ni baada ya watafiti kugundua uwepo wa volkano iliyo hai "Mawson's" pia zuio la kutembelea sehemu hiyo lilitokana na hali ya hewa pamoja na suala la kiusalama.


3. Ilha da Queimada Grande, Brazil
 
Kinafahamika kama kisiwa cha nyoka, ni makazi ya nyoka wakubwa kuwahi kupatikana, imeelezwa kuwa kila baada ya hatua moja kuna nyoka mmoja ndani ya kisiwa hicho, na nyoka wanapatikana katika kisiwa hicho wakiwemo nyoka wenye vichwa vya dhahabu ndio nyoka hatari zaidi duniani.

Kutokana hali hiyo Serikali nchini Brazil wamekifunga kisiwa hicho kwa watalii ni watafiti wenye uelewa wa nyoka wakiambatana na timu ya madaktari ndio wanaoruhusiwa kuingia katika kisiwa hicho.



4. Ngome ya Bhangarh, India

Inapatikana katika Wilaya ya Alwar nchini India ikiwa ni kilomita 220 kutoka mji wa Delhi, inaeleza kuwa ilianza kujulikana tangu miaka 400 iliyopita na imeruhusiwa kutembelea eneo hilo nyakati za mchana pekee na hiyo ni kutokana na hadithi za vizuka na laana zinazosimuliwa kutoka maeneo hayo.

Ngome hii ilijengwa mwaka 1573 na Raja Bhagwatant Das  ambaye alikuwa mtawala wa Amber Kachwaha kabla ya kuanguka kutokana janga la njaa la mwaka 1783.



5. Poveglia, Italia

Poveglia ni kisiwa kidogo kinachopatikana kati ya Venice na Lido na katika miaka ya nyuma ilikuwa karantini ya kukabiriana ugonjwa wa tauni,  watu  zaidi ya milioni 160 walioambukizwa homa ya tauni  waliishi huko wakisubiri siku zao za mwisho, na inaelezwa kuwa asilimia 50 ya mchanga wa kisiwa hicho una mabaki ya binadamu hata hivyo baadaye kisiwa hicho kikawa hospitali ya magonjwa ya akili na kupata sifa mbaya zaidi iliyopelekea kufungwa na hatimaye kupigwa marufuku kutembelewa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...