Lebanon inaomboleza baada ya mlipuko mkubwa katika mji mkuu wa Beirut kuwaua watu 78 na kuwajeruhi wengine 4000 siku ya Jumanne.
Mji wote uliyumbishwa na mlipuko huo, ulioanza kwa moto katika bandari kabla mlipuko huo uliofanana na wingu la uyoga kutokea.
Rasi Michel Aoun alisema kwamba tani 2,750 za ammonium nitrate zilikuwa zimewekwa vibaya katika ghala moja kwa miaka sita.Aliitisha kikao cha dharura siku ya Jumatano , na kusema hali ya dharura ya wiki mbili imetangazwa.
Rais
Aoun pia alitangaza kwamba serikali itatoa $66m za hazina ya dharura.
''Kile tunachoshuhudia ni janga kubwa'' , alisema mkuu wa kundi la
msalaba mwekundu George Kettani akizungumza na vyombo vya habari. ''Kuna
waathiriwa kila mahali''.
Maafisa walisema siku ya Jumanne kwamba uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo kilichosababisha mlipuko huo.Baraza kuu la ulinzi nchini Lebanon lilisema kuwa wale waliohusika wataadhibiwa vilivyo.
Ammonium Nitrate ilikuwa imeshushwa kutoka kwa meli iliokamatwa katika bandari hiyo 2013 na kuwekwa katika ghala.Mlipuko
huo unajiri wakati mgumu kwa upande wa taifa hilo , huku likikabiliwa
na mgogoro wa kiuchumi unaosababishwa na mgawanyiko wa jadi huku taifa
hilo likiathiriwa na mgogoro mwengine wa virusi vya corona.
Hali ya wasiwasi pia iko juu kabla ya uamuzi wa siku ya Ijumaa kuhusu kesi ya mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu Rafik Hariri 2005.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...