Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi na Mwekezaji wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'MO' amesema kuwa kiasi cha Shilingi Bilioni 20 za Kitanzania tayari zimewekwa klabuni hapo kama makubaliano ya uwekezaji yalivyokuwa.
MO ameyasema hayo kupitia Kipindi cha Michezo cha Wasafi TV, amesema kila mwaka anatoa zaidi ya Bilioni 3 kufidia Mishahara, Usajili nk, amesema Bilioni 20 hizo zinatolewa kwa utaratibu wa kipindi cha mpito 'transition.
Pia, MO Dewji amebainisha kuwa hawezi kuondoka klabuni hapo licha ya jumbe anazoziandika katika kurasa zake za Mitandao ya Kijamiii ikiwemo 'Twitter', amesema kuna baadhi ya watu wanataka kuivuruga klabu hiyo kwa uvumi usiokuwa na tija ndani yake.
"Mimi nimewekeza Bilioni 20 Simba SC sasa naondokaje?, baada ya kuweka hela yote hiyo?
" amehoji Mo Dewji.
Kuhusu mabadiliko ya Logo ya Klabu hiyo, MO amesema wamebadilisha baada ya kufanya utafiti na kuona mabadiliko ya Logo, Slogan za timu zaidi ya 1000.
Kuhusu kuleta timu kubwa kwenye Tamasha la Simba Day, MO ameeleza kuwa ana marafiki wengi barani Ulaya hivyo Matamasha ya baadae linaweza kutokea lolote kwa ujio wa timu kubwa kutoka Ulaya.
Baada ya kuondoka Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu, Senzo Mbatha, MO amesema wako kwenye mchakato wakupata CEO mwengine licha yakuondoka Senzo, amesema watahakikisha wanapata mtu mwengine mwenye mapenzi na timu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...