Msaada wa vyakula, nguo na mahitaji mbalimbali ambayo mashabiki wa Liverpool jijini Dodoma wamepeleka katika Kituo cha watoto wenye uhitaji cha Kijiji cha Matumaini ikiwa ni kusheherekea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya England
 Naibu Waziri wa Kazi Ajira na Vijana, Anthony Mavunde Akizungumza katika tukio la kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na mashabiki wa Liverpool jijini Dodoma leo kwa Kituo cha watoto wenye uhitaji maalum cha Kijiji cha Matumaini.
 Naibu Waziri wa Kazi Ajira na Vijana, Anthony Mavunde akikabidhi baadhi ya mahitaji kwa watoto wa Kituo cha Kijiji cha Matumaini ambayo yametolewa na mashabiki wa Liverpool jijini Dodoma leo.
 Mwenyekiti wa Mashabiki wa Liverpool jijini Dodoma, Abraham Gama Akizungumza kwa niaba ya mashabiki wa Timu hiyo katika tukio la kukabidhi msaada wa mahitaji mbalimbali kwa kituo cha watoto wenye uhitaji cha Kijiji cha Matumaini leo.

Charles James, Michuzi TV
KATIKA kusheherekea ubingwa wa Ligi Kuu ya England mashabiki wa Liverpool jijini Dodoma, wametembelea Kituo cha watoto wenye uhitaji cha Kijiji cha Matumaini na kutoa misaada mbalimbali kwa watoto hao.

Katika tukio hilo mashabiki hao wameongozana na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira, Anthony Mavunde ambaye amewataka mashabiki wa timu zingine ikiwemo za hapa nchini kuwa na moyo wa kusaidia watu wenye uhitaji.

Naibu Waziri Mavunde amesema licha ya yeye kuwa shabiki wa Manchester United ambao ni wapinzani wa Liverpool lakini ameguswa kuungana na mashabiki hao kutokana na moyo wao wa kusheherekea furaha yao kwa kupeleka mahitaji mbalimbali kwa watoto hao.

" Niwapongeze sana ndugu zangu wa Liverpool kwa moyo wenu wa upendo, mngeweza kuchanga fedha zenu na mkafanya sherehe kwa kunywa pombe lakini mmeona ni vema mlete mahitaji kwa watoto hawa, Mungu awabariki na iwe rai kwa mashabiki wa timu zingine kufanya tukio la kizalendo kama hili," Amesema Mavunde.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashabiki hao, Abraham Gama amesema wao kama mashabiki wameona washeherekee ubingwa wao kwa kuwaletea watoto hao mahitaji mbalimbali ikiwemo vyakula, pampers, mafuta ya kupikia, sabuni, nguo na maziwa ambayo yote ina gharama ya Sh Milioni Moja.

Nae Katibu wa Mashabiki hao, Charles James amewashukuru wadau mbalimbali waliojitolea kufanikisha tukio hilo ikiwemo Kampuni ya Matairi ya Binslum Tyres na Kampuni ya Maziwa ya Tanga Fresh.

" Hili ni tukio endelevu na tumepanga uwe utaratibu wa mashabiki wa Liverpool Dodoma kusaidia watu wenye uhitaji mara kwa mara, Liverpool ni Klabu inayothamini utu na yenye kujali watu wenye uhitaji tutaendelea kusaidia wenye uhitaji hata bila kusubiri kutwaa ubingwa," Amesema James.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...