Na Bakari Madjeshi,  Michuzi TV

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Mhe. Abubakar Kunenge amemtaka Mkandarasi na Msimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa Stendi ya Mabasi Mbezi kukamilika kwa wakati ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu.

RC Kunenge ametoa agizo hilo wakati akikagua ujenzi wa Miradi mbalimbali ndani ya jiji hilo la Dar es Salaam.

Kunenge amesifu jitihada za Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo kufuatilia kwa karibu ujenzi wa mradi huo, amesema ametembelea mradi huo mara kwa mara tangu alipokuwa RAS chini ya Uongozi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.

"Tuwe na uhakika wa kumaliza mradi huu kwa wakati,  kwanza tunajivunia kuwa na mradi mkubwa miongoni mwa miradi mikubwa ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini Rais wetu,  Dkt. John Pombe Magufuli.

Pia,  RC Kunenge ameshauri kuhakikisha kukamilika kwa maeneo muhimu katika eneo hilo,  maeneo kama Hotel kwa ajili ya watu kufika na kulala eneo hilo.

Hata hivyo, amewataka Wasimamizi wa Mradi huo kufikiria juu ya uongozi kwa ajili ya kuendesha mradi husika. " Hapa anatakiwa Mtaalamu haswa,  tushauriane viongozi ili kupata Mtaalamu wa kuendesha".

"Mkuu wa Wilaya na Katibu Tawala Wilaya (DAS) wa Ubungo hakikisheni mnafuatilia kwa karibu na mara kwa mara ujenzi wa mradi huu",  ameagiza Kunenge.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...