Na Zainab Nyamka, Michuzi TV.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar Es Salaam Abubakar Kunenge amewaagiza Mamlaka ya
Majjsafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuhakikisha
wanapeleka miradi mikubwa ya maji katika maeneo yenye wakazi wengi.
Akizungumza
na Menejimenti nzima ya Mamlaka hiyo ikiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu
Cyprian Luhemeja, amesema kuwa Dawasa wanatakiwa wasijilinganishe na
taasisi zingine bali wanatakiwa wafike kimataifa.
Kunenge amesema, naifahamu Dawasa kwani nilishakua hapa wakati wa dawasco nafahamu changamoto zilizokuwa zinakuta ila kwa sasa
mkoa wa Dar es Salaam mmejitahid na mmefanya kaz kubwa na ni miongoni mwa taasisi zilizofanya kazi vizuri.
"Nilifanya
ziara maeneo ya Pugu, wananchi walitoa malalamiko katika sekta ya maji
ila mwakilishi wenu kutoka Kisarawe alielelezea kuna mradi kutoka
Kisarawe hadi Pugu wananch walifarijika sana," amesema Kunenge.
Amesema,
Dawasa wana kazi kubwa ya kufanya ikiwemo kutoa taarifa kwa wananchi
wafahamu mradi umefikia wapi na lini utakamilika ili kutatua changamoto
ya maji.
"Najua mmejipanga
vizuri, miradi hiyo inayotekelezwa iondoe changamoto kwa wananchi na
mhakikishe hadi kufikia wakati wa uchaguzi changamoto ziwe
zimekamilika,"amesema
Kunenge amesisitiza kuwa, Dawasa
hawafanyi Biashara ila wanatoa huduma kwa wananchi na mnapopata mapato
mengi basi fedha hizo zinaenda katika uwekezaji wa miradi hususani
kwenye maeneo yanayoendelea kukua kwa kasi.
"Maeneo
ya Kigamboni na Mwabepande, ni maeneo ambayo yanaendelea kukua zaidi
kwani mkakati wa serikali ni kuona mkoa wa Dar es salaam unakuwa mkoa
wa uwekezaji" amesema.
"Nafarijika
nasikia nchi nzima wanatumia kauli ya mtue mama ndok kichwani kwan
najua ilianzia hapa na mnatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi ya
kutatua changamoto ya maji",
Mkuu
wa Mkoa ahadi ya kutembelea miradi yote ya Dawasa pamoja na kutembelea
maeneo yenye changamoto kubwa ya maji ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Aidha,
ametoa pongezi kwa Mtendaji Mkuu wa Dawasa kwa kazi kubwa anayoifanya
ya kutekeleza miradi ya Dasawa kwa fedha Za ndani tofauti na zamani
ambapo walikuwa wanasakamwa kwa madeni makubwa.
Naye
Mtendaji Mkuu, Mhandisi Luhemeja amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuja
kuwatembelea pamoja na kutoa maagizo yake ambapo wameahidj kuyatekeleza
kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abuubakar Kunenge
akizungumza na wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira
Dar es Salaam DAWASA baada ya kuwatembelea katika ofisi zao Jijini Dar
es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka
ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA Mhandisi Cyprian
Luhemeja akitoa taarifa fupi ya miradi inayotekelezwa na Mamlaka hiyo
kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abuubakar Kunenge baada ya kuwatembelea katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam.
Wakurugenzi mbalimbali wa Mamlaka
ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA wakimsikiliza
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abuubakar Kunenge baada ya kuwatembelea katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...