Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo.
Mwili wa marehemu tayari umekwisha kusafirisha kwenye uwanja wa ndege
Mkoani Tanga na kuelekea visiwani humo na mazishi yake yanatarajiwa
kufanyika leo Jioni kwenye eneo la Fuoni Unguja kisiwani Zanzibar.
Akizungumza jana Mtoto wa Pili wa Marehemu Moyo,Mohamed Moto alisema kwamba mwili wa baba yake ulisafirishwa leo saa tatu asubuhi kwa ndege na kufikishwa visiwani Zanzibar kwa ajili ya mazishi.
Mohamed ambaye pia ni katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya
Muheza alisema baba yake alikimbizwa hospitali ya Bombo usiku wa
kuamkia jumanne Agosti 17 mwaka huu kutokana na kuugua ghafla kifua na
kubana pumzi ambayo haikuwa ikitoka vizuri.
“Baba hakuwa akiugua na hakuugua kwa muda mrefu…alianza kubanwa na
kifua na baadaye akaanza kupata shida ya kupumua ilipofika saa 7.00
usiku ndipo akafariki”alisema Mohamed.
Alisema Mzee Moyo atazikwa leo jumanne saa 10.00 jioni nyumbani kwake
Fuoni Zanzibar.
Inna lillah wainna ilayhi rajiuna.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...