Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv.
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeifungia matangazo Clouds TV na Clouds Redio kwa wiki moja kuanzia leo Agasti 27 hadi Agasti 3 mwaka huu.
Sambamba na kufungiwa kuanzia leo na kesho ya Agasti 28 katika vituo hivyo kazi yao ni kuomba radhi Umma kwa kitendo walichokifanya.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 27,2020 ijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Mhandisi James Kilaba amesema katika vipindi vya 360 na Power Breakfast walirusha takwimu za wgombea ubunge waliopita bila kupingwa wakati taarifa hiyo haijadhibitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) na kukosa mezania.
Mhandisi Kilaba alimnukuu Mtangazaji "Sasa kuna wagombea ambao wamepita bila kupingwa ...mimi nilikuwa ninazo 23 mpaka saa hizi (kumi na nane zikaongezekaje hizo zingine)...si watu wanazidi ku-confirm (kwa hiyo kuna uwezekano kwamba zinaweza kuzidi)...zinaweza kuzidi ...
"Ishapita kwa sababu ,aaah mpaka saivi ,mpaka tunaingia mtamboni hapa ...23 washafika..."
Amesema kifungu cha 16 (1) cha kanuni za Utangazaji (Maudhui) na kanuni ndogo za utangazaji wakati wa uchaguzi za mwaka 2015 zimebainisha wajibu wa mtoa maudhui kutoa taarifa za matokeo ya uchaguzi kwa kadri zinavyopatikana na kutolewa na Tume ya Uchaguzi na kuhakikisha matokeo yanatangazwa kwa ufasaha .
Mkurugenzi Mkuu Kilaba amesema mtoa huduma ya maudhui anapaswa kufuata kanuni,Sheria na masharti ya leseni sambamba na maelekezo yanayotolewa na mamlaka .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...